Header Ads Widget

WAZIRI LUKUVI ATEMBELEA VYAMA VYA SIASA, ATOA WITO HUU

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na uratibu William Lukuvi leo amefanya ziara ya kuvitembelea vyama vya siasa ikiwa ni lengo kujitambulisha kwa viongozi wa vya hivyo sambamba na kuhamasisha ushiriki wao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 



Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo ambapo ametembelea Chama Cha Ukombozi wa Umma (Cha Umma), Act Wazalendo, Chama Cha Kijamii (CCK) na Chama Cha United People Democratic Party (UPDP) ambapo amewasihi kudumisha upendo na kufata falsa ya 4R za Rais Dkt Samia wanapoelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.



Amesema kuwa, ameanza na utaratibu mpya wa kuwafuta viongozi wa vyama vya siasa ofisini kwao badala ya kukutana navyo kupitia mgongo wa msajili wa vyama vya siasa Jaji Fransc Mutungi ambapo lengo lake ni kuvitembelea vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu.



"Leo nimetembelea vyama hivi vinne na kesho pia nitatembelea vyengine vinne, baada ziara ya kesho nitasitisha kidogo ratiba hii Kwa sababu kuna mkutano wa baraza la vyama vya siasa utakaofanyika Dodoma na mimi natakiwa niwepo"amesema Waziri Lukuvi.


Hata hivyo, amewataka  viongozi na wananchi wote kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa utakao anza mapema mwezi Novemba ili wapate fursa ya kupiga kura na kuchagua kiongozi wanaemtaka ambapo zoezi la uandikishaji litaanza tarehe 11hadi 20 mwezi huu.


Aidha,  Waziri Lukuvi akijibu hoja ya Kiongozi wa chama Cha ACT -Wazalendo Dorothy Semu amesema kuwa Rais Dkt Samia ameahidi uchaguzi utakaofanyika chini ya uongozi wake utakua wa huru na haki ambao utafuata kanuni, sheria na taratibu walizokubaliana, hivyo hakuna mwananchi atakaepata vitisho kutoka kwa viongozi.


Awali, kiongozi wa Chama Cha ACT -Wazalendo alisema wanapokwenda kuwahamasisha watu kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa wamekua wakipokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao, ambapo wamesema wamekuwa wakipokea vitisho kutoka kwa watendaji na viongozi mbalimbali jambo ambalo limeanza kuwapa hofu juu uchaguzi huo.


Mohammed  Massoud Rashid ni Katibu Mkuu wa chama Cha Umma amesema watashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani wameona mabadiliko makubwa ukilingalisha walipotoka toka kisiasa na walipo, hivyo wanaendelea kuhamasisha wananchi wajitokeze wa wingi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama Cha Kijamii (CCK) David Daud Mwaijojewe amesema licha ya kujipanga vyema kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuhamasisha wananchi kushiriki lakini wanakabiliwa na ukosefu wa ruzuku hali inayopelekea kujiendesha kwa kusuasua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI