Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Jumla ya mashuka 150 yenye thamani ya shilingi milioni 2.4 yamekabidhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe toka kwa watumishi wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO kupitia Saccos ya shirika hilo.
Akikabidhi Mashuka hayo Mwenyekiti wa SACCOS Hiyo Bwana Sostenes Kateule amesema umekuwa ni utaratibu wa kawaida kurejesha fadhira kwa Jamii kutokana na Faida zinazopatikana katika Saccos Yao na kwamba yatasaidia kupunguza baadhi ya Changamoto kwa wagonjwa.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe Dokta Gilbert Kwesi amesema mashuka hayo yatasaidia kuokoa baadhi ya fedha zilizotakiwa kununua mashuka katika awamu nyingine na kwamba zitafanyakazi nyingine za uboreshaji huduma.
Sanjari na Hayo lakini pia Dokta Kwesi amewataka wananchi kutumia Hospitali yao kwa kuwa tayari inao madaktari Bingwa hadi wa Upasuaji wa Ubongo.
Baadhi ya wananchi Mkoani Njombe akiwemo Rehema Mwalongo na Prisca Ndone licha ya kupokea kwa mikono miwili msaada wa mashuka hayo lakini wanasema kwa sasa huduma zimeboreshwa katika Hospitali hiyo tofauti na kipindi kilichopita.
0 Comments