Header Ads Widget

POLISI YAZINDUA KAMPENI KUKABILI UKATILI SHULENI VYUONI.

KAMPENI ya Kupinga Ukatili inayofanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Pwani iitwayo Tuwaambie kabla Hawajaaribiwa inatarajia kuwafikia wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari 12,927.


Aidha kampeni hiyo ya utoaji elimu kwa shule hizo 139 pia itawafikia wanafunzi wa vyuo wapatao 1,968 kwa mkoa huo.


Akizindua kampeni hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani (SACP) Pius Lutumo amewataka wanafunzi wasibadilike kutokana na mazingira ili wasije kuingia kwenye vitendo vitakavyosababisha kuendelea vitendo vya ukatili.


Lutumo amesema kuwa kampeni hiyo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo imelenga kundi hilo kwani ndilo limekuwa likibadilika kutokana na mazingira wanayokutana nayo.


Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Jamii (ACP) Michael Manumbu amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia jamii kuwa na vijana wenye maadili mazuri ili waweze kufikia ndoto zao ambazo wajiwekea.


Naye Mkurugenzi wa Kuhani Mussa Media Group Joshua Kisaka amesema kuwa wameanzisha kampeni ya kuzuia mmomonyoko wa maadili ili kulinda kizazi kijacho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI