Header Ads Widget

MZEE MALECELA NA MKEWE ANNE KILANGO MGUU KWA MGUU JIMBONI SAME MASHARIKI..

 


NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara na Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Malecela ameongozana mguu kwa mguu na mkewe Anne kilango Malecela Mbunge wa Jimbo la Same mashariki kutembelea kijiji cha Makokane kata ya Kalemawe. 


Lengo la ziara hiyo ni kuona juhudi za wananchi wa kijiji hicho katika kujiletea Maendeleo bila kusubiri fedha za serikali ambapo juhudi hizo zimemkosha sana Mzee Malecela na kuwiwa kuwachangia fedha milioni 1.5.


Aidha Mzee Malecela aliwasihi waendelee kuwa wamoja na mshikamano  kwani zahanati hiyo inakwenda kuwa mkombozi wao na kwa kizazi kijacho. 


Pia aliwaomba waendelee kuiunga mkono serikali ya Chama cha mapiduzi inayoongozwa na Jemedari Daktari Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. 


"Mimi pamoja na mbunge wenu tuko bega kwa bega na ninyi kuhakikisha tunawaunga mkono juhudi zenu na tutaendelea kuwaunga mkono katika mambo ya maendeleo" Amesema Mzee Malecela. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI