Header Ads Widget

DCP MISIME -WAANDISHI WA HABARI FANYENI KAZI KWA USHIRIKIANO NA JESHI LA POLISI

 


MSEMAJI  wa Jeshi la Polisi nchini, DCP David Misime katikati aliyekaa akiwa na baadhi ya wanahabari nchini na washiriki wa kongamano la Kitaifa la Aman lililoandaliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kufanyika Leo jijini Dar es Salaam wa kwanza kushoto mkurugenzi wa UTPC Keneth Simbaya

Na Matukio Daima App 

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, DCP David Misime, amewataka waandishi wa habari na polisi kufanyanyq kazi kwa ushirikiano na weledi na Kila mmoja kuzingatia mipaka ya kila mmoja kitaaluma ili kujenga taifa imara.


DCP Misime amesema hayo, katika kongamano la amani lililojumuisha waandishi wa habari na jeshi la polisi, lililokuwa na lengo la kukumbushana majukumu ya pande zote mbili.

Amewakumbusha waandishi wa habari kuzingatia usalama wao, pindi wawapo kazini ili kujiepusha na madhara yanaweza kujitokeza ikiwemo kuzingatia uvaaji wa vizibao vya utambulisho pamoja na kuacha kuandika habari za uchochezi ama hatarishi.

"Lazima tuzingatie usalama, na ndiyo maana tulisisitiza vyombo vya habari lazima viwe na sesheni ya mambo ya ulinzi kama uwepo wa vizibao (press code) usiende kwa kificho hata kama unaandika habari za uchunguzi zingatia usalama waka" alisema DCP David Misime.


Pia amewakumbusha wanahabari kuwa na uwezo wa kutambua habari ambazo zinahitaji kuachwa kwa maslahi mapana ya taifa na vizazi vijavyo.

"Hii ni nchi yetu lazima tuijenge, tunahitaji kuwa na mazingira salama siku zote na sisi ndiyo tunao mpira sasa hivi, sisi ndiyo wenye uwezo wa kuijenga Tanzania Imara" Alisema DCP Misime.

Katika hatua nyingine, amewakumbusha viongozi wa vilabu vya waandishi wa habari nchini, kuendelea kutoa elimu mara kwa mara kwa wanachama wao ili waandishi waendelea kusimamia taaluma zao pamoja na kudumisha amani.

DCP Misime amesema kwa sasa jeshi la polisi limekuwa likitoa elimu kwa askari wao katika idara mbali mbali ili kuendelea kulijenga zaidi.

"Sisi tunaelimisha askari wetu sana, sheria mbali mbali, matamko na namna ya kushughulika na jamii, wametoka huko vyuoni wamekariri vitu atapata shida na atagombana na watu sana"Alisema DCP Misime.


Kupitia  mjadala wa nini nini kifanyike kupunguza Matukio ya waandishi wahabari nchini kukamatwa na polisi  Mwanahabari huyo alisema kuwa Bado Kuna haja ya polisi kutoa majibu sahihi ya waandishi hao kukamatwa .


Akijibu hoja hizo DCP Misime alisema kuwa polisi hawakamati bila sababu lazima kamatakamata yoyote Ina sababu yake.

Kuhusu Suala la waandishi wawili waliodaiwa kukamatwa kwenye maandamano ya CHADEMA leo alisema hata weza kutolea majibu Kwa sasa pasipo kujua sababu ya kukamatwa kwao .

Japo alisema si kosa kwa waandishi wa habari kuripoti habari za maandamano na ndio maana hakuna sehemu yoyote ambayo jeshi la polisi limetoa Kauli ya Kuzuia waandishi kuripoti maandamano nchini .

DCP Misime alisema kuwa jeshi la polisi linafanya kazi kwa weledi na kuwa hawafanyi kazi kwa mihemuko wala kutekeleza maelekezo ya Chama chochote Cha siasa .

Aidha alisema ku


wa Suala la polisi Service litaendelea kufanyiwa kazi zaidi kama ambavyo Mheshimiwa Rais alivyoelekeza.

Alisema wataendelea kuendeleza na kuwekeza mkazo wa Polisi jamii pamoja na kupeleleza Kesi kwanza kabla ya kukamata .

Japo alisema Kesi ya uhujumu uchumi,uhaini ,mauaji na Kesi nyingine kubwa hawatasubiri upelelezi ndipo wakamate watakamata haraka zaidi ila Kesi za matusi na nyingine zisizo na madhara makubwa hizo watafanyavuchunguzi .

Katika hatua nyingine DCP Misime alisema jeshi hilo litaendelea kutangaza watuhumiwa wote wanaofungwa jela kama njia ya kupunguza Matukio ya uhalifu nchini.

Kwani alisema kuendelea kukamata watuhumiwa bila Kuwepo mrejesho wa hukumu zao hakutasaidia kupunguza Matukio ya uhalifu na kuwa toka wameanza kutangaza watuhumiwa wanaofungwa jela Matukio ya uhalifu mkubwa yameendekea kupungua isipokuwa Matukio yanayowasumbua Kwa sasa ni yale ya mmomonyoko wa maadili .

Katika taarifa yake kwa umma kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ilisema kuwa waandishi wake wawili kwa nyakati tofauti walikamatwa wakati wakiripoti maandamano ya amani yaliyoitishwa na Chadema. 

Hata hivyo mmoja amekwisha achiwa Hadi Kuwa hadi sasa jeshi hilo linamshikilia Lawrence Mnubi ambaye ni mpiga picha jongefu (videographer) wa Mwananchi, aliyekuwa eneo la Msimbazi akitimiza wajibu wa kuhabarisha umma, akiwa na kitambulisho na vifaa vya kazi.

Wakati asubuhi ya leo Jumatatu Septemba 23, 2024, mpigapicha wa Mwananchi, Michael Matemanga alikamatwa na polisi eneo la Buguruni.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI