Header Ads Widget

VIONGOZI NA WAFUASI WA CHADEMA 14 WAKATWA DAR ES SALAAM



Na Matukio daima App,


Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SCAP. Muliro Jumanne Muliro, leo Jumatatu Septemba 23, 2024  amesema Jeshi la Polisi limewakamata watu 14 wakiwemo baadhi ya viongozi wa Chadema ambao ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti, Tundu Lissu pamoja na Mwenyekiti wa kanda ya kaskazini Godbless Lema.


Kamanda Muliro amesema watu hao wanaendelea na mahojiano huku ukamataji huo unakuja, kufuatia katazo lililotolewa na wakalikaidi.


Aidha amewataja wafuasi wengine waliokamatwa na jeshi hilo kuwa ni, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Rhoda Kunchela, Peter Lazaro, Sheikh Omary Faki, Revocatus Mlai, Paulo Musi, Shabani Mabela, Aboubakari, Emmanuel, Silvester, Mary Nugu, na Bakari Habibu Salum.

Kamanda Muliro amewaambia waandishi wa habari kuwa, doria ya polisi iliyoonekana leo itakuwa endelevu katika mitaa mbalimbali nchini hivyo kuwa toa hofu wananchi.

Watu wema wanaotaka amani wanafurahi sana kuiona hiyo mitutu Barabarani, wanaohofia kuwaona maaskari Barabarani ni wahalifu, hivyo Doria zitadumu sana”.

Katika hatua nyingine Kamanda Muliro amesema, jeshi la Polisi lilifatilia matamko mbalimbali ya Chadema na kubaini uwepo wa matamko yalikuwa na viashiria vya kufanyika kwa maandamano yasiyokuwa ya amani. 

"Hatukuhitaji kusubiri kuona maandamano Barabarani ndio tudhibiti, tusingeweza kusaidia madhara ambayo yangetokea ndio maana tumewazuia” Kamanda Muliro.


Hata hivyo, Kamanda Muliro amekanusha kukamtwa kwa mtoto wa Freeman Mbowe, Nicole Mbowe ambaye mapema leo eneo la Magomeni mapipa alionekana akipandishwa kwenye gari la polisi, baada ya kukamatwa kwa baba yake  na kusema kuwa waliokamatwa ndiyo aliyowataja.

Akijibu swali la Mwaandishi wa habari kamanda Muliro alisema “Nimetaja waliokamatwa, nadhani jibu lake umeshalitambua”.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI