Na Mwandishi Wetu,Kigoma
Francis Jackson (26) Mkazi wa Murusi wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kutoroka mahakamani chini ya ulinzi wa polisi alipokuwa aMeshitakiwa kwa wizi wa pikipiki mali ya Halmashauri ya wilaya Kasulu iliyotolewa na Raisi Samia Suluhu Hassan kwa watendaji wa idara ya kilimo ya halmashauri hiyo.
Ilielezwa mahakamani hapo na Wakili Mwandamizi wa serikali, Happiness Mayunga kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 10 mwaka huu majira ya mchana katika mahakama ya wilaya Kasulu.
Mayunga alisema kuwa Mshitakiwa alitenda kosa hilo baada ya kufikishwa mahakamani hapo akishitakiwa kwa kosa la wizi wa pikipiki mali ya idara ya kilimo ya Halmashauri ya wilaya Kasulu.
Iilielezwa mahakamani hapo kuwa Siku ya tukio, Mshtakiwa alikuwa ametoka Mahakamani kusomewa hoja za awali za
kosa la Wizi wa Pikipiki aina ya Boxer , yenye Engine Na.*PFXWNE3505 ambayo ilikuwa bado haijasajiliwa
linaloendelea mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Immaculate Shuli ambapo aliamriwa kurudishwa remande baada ya kukosa dhamana.
Mayunga alisema kuwa Wakati Mshtakiwa anapanda gari la Polisi kurudishwa rumande ndipo akaruka kwenye gari na kukimbi ambapo hata hivyo alikamatwa umbali mchache baada ya kukimbia mikononi mwa polisi.
Kufuatia kosa hilo na Mshitakiwa kukiri kosa Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya wilaya Kasulu , Imani Batenzi alimuhukumu mshitakiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani ili kuwa fundisho kwa washitakiwa wengine wenye nia kama hiyo.
Mwisho.
0 Comments