Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
MWENYEKITI wa UWT Taifa, Marry Chatanda amesema Baraza kuu la umoja wa wanawake Tanzania litaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dk.Samia katika kutekeleza miradi yote ya kimkakati.
Pia baraza hilo la (UWT) limempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uzinduzi wa huduma za safari za treni ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salam hadi Dodoma.
Akitoa tamko hilo jijini hapa mwenyekiti huyo amesema Baraza limesema mradi huo utasaidia kupunguza ajali, msongamano na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania.
"Baraza la UWT Taifa tunatoa tamko la kumpongeza Rais Dk. Samia kwa kuzindua safari za treni ya umeme ya SGR kutoka Dar es Salam hadi Dodoma ambayo inatuma saa tatu. Hii ni ishara tosha kuwa yeye si mtu wa maneno bali vitendo kwasababu aliahidi kukamilisha miradi yote waliyoiasisi wakiwa na mtangulizi wake hayati Dk.John Magufuli,"amesema
Ameongeza kuwa:"Kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza foleni, kufungua fursa za kiuchumi na kuongeza upatikanaji wa ajira kwa Watanzania,"
Amesema UWT inatoa wito kwa wananchi wanaozunguka mradi huo wa kimkakati kuhakikisha wanaendelea kulinda na kutunza miundombinu ili ilete manufaa kwa Taifa.
0 Comments