Header Ads Widget

NCHIMBI ATAKA AHADI ZA RAISI SAMIA KIGOMA ZITEKELEZWE

 

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

Katibu Mkuu wa CCM Emanuel Nchimbi ameitaka serikali kuhakikisha inatekeleza na kukamilisha miradi yote ambayo imeahidiwa na Raisi Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuufungua mkoa Kigoma ili kuufanya mkoa wa kimkakati wa uchumi na biashara.

Nchimbi alisema hayo akihutubia Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma.

 

Kutokana na hilo alisema kuwa  ahadi ya Raisi ya ujenzi wa mbili katika ziwa Tanganyika zinazolenga kuufanya mkoa huo kuwa rahisi kuingia na kutoka mkoani humo na hiyo inalenga kuongeza mzunguko kwenye suala la uchumi hivyo meli hizo zikamilike kulingana na ahadi zilizotolewa.

 

Sambamba na hilo alisema kuwa ipo miradi ya vituo vya kupoza umeme ili kuondoa tatizo la umeme mkoani Kigoma naomba ahadi hiyo ikamilishwe hadi kufikia mwezi machi mwakani kama ahadi ilivyotolewa huku akihimiza kukamilishwa kwa miradi ya barabara za viwango vya lami.

 

Katibu Mkuu Nchimbi alieleza kuhusu utekelezaji wa treni ya kisasa iendayo kasi (SGR) kwamba kukamilika kwa mradi huo kutabadilisha na kuinua shughuli za uchumi za mkoa Kigoma jambo ambalo ni ndoto kubwa ya Raisi Samia kuona mkoa Kigoma unapiga hatua kubwa kimaendeleao kwani Trilioni 11.4 alizoleta mkoani humo zinaoonyesha mapezni yake ya kweli kwa wananchi wa mkoa huo.

 


Kufuatia hali hiyo Nchimbi amekipongeza Chama cha Mapinduzi na serikali ya mkoa Kigoma kwa kusimamia utekelezaji wa miradi inayotokana na fedha hiyo ya serikali kiasi cha shilingi trilioni 11.4 na kusema kuwa miradi hiyo inaonekana ktekelezwa kwa viwango vizuri na hivyo kuwataka wananchi wa mkoa Kigoma kumuombea Raisi Samia  ili utumishi wake kwa umma uendelee kutukuka kutokana na anavyotafakari umasikini wa Watanzania.

 

Awali akizungumza mbele ya Katibu  Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa miaka mitatu ya Raisi Samia madarakani serikali imepeleka mkoani Kigoma kiasi cha shilingi Trilioni 11.4 kwa nia  ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa katika fedha hizo zimekuja kutekeleza miradi mbalimbali na tayari miradi yote ambayo imeahidiwa na Raisi Samia imeanza kupatiwa fedha na miradi yote imeanza kutekelezwa.


Katika ziara yake Kigoma Mjini Katibu Mkuu wa CCM amevuna wanachama zaidi ya 250 kutoka vyama vya upinza wakiongozwa na aliyekuwa mbunge Mstaafu wa viti maalum CHADEMA, Sabrina Sungura na  Diwani wa kata ya Mwakizega kutoka chama cha DP huku akisikiliza kero 55 za wananchi 38.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI