NA THABIT MADAI- ZANZIBAR matukiodaima3@gmail.com
CHAMA cha Act Wazalendo kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia suluhu Hassan kuharakisha utekelezaji wa ripoti ya haki jinai ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi kwa misingi ya haki na Uweledi.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othaman kufuatia Tamko lililotolewa hivi karibuni na Kamshna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad la kuwataka viongozi wa siasa kuacha kutumka vibaya uhuru kwa kutoa kauli matusi na kebehi kwa viongozi wa Serikali na vyama vya siasa.
Amesema hatua hiyo ya Rais Dkt. Samia itasaidia kufikia lengo lake la kulifanyia mageuzi Jeshi la Polisi na kufanya kazi kwa uwadilifu na haki.
"Tunamuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuongeza msukumo na kuharakisha utekelezaji wa ripoti ya Tume ya Haki jinai nchini ili kufikia lengo lake alilolitaja hadharani na kuwahidi watanzania kwamba jeshi la Polisi litafanyiwa mageuzi makubwa," amesema.
"Miongoni mwa kasoro kubwa za kimfumo wa Utekelezaji wa haki za polisi unaohitaji mageuzi ya haraka ni ule hasa ngazi za mikoa kuchukua amrita za kisiasa kwa masuala ya haki za watu kutoka kwa wakuu wa mikoa na wilaya ambao baadhi yao so waadilifu,wanakiuka katiba na sheria za nchi katika utendaji wao," amesema.
Mwenyekiti huyo ambae ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa misingi iliyoweka na kuacha kuegemea upande mmoja wa kisiasa.
"Jeshi la Polisi bado wanayo nafasi ya kufanya kazi zao kwa uadilifu, hivyo liache kujiegemeza upande mmoja wa siasa, amesema
Hata hivyo ameeleza kuwa chama hicho kitasamia maoni ya Wanachi ya kutoshirikia uchaguzi Mkuu kwa siku mbili.
Mkutano na Waandishi wa Habari umefanyika katika ofisi ndogo za chama hicho Vuga Mjini Magharibi Unguja.
0 Comments