Na Matukio Daima Media, Dar es Salaam
matukiodaima3@gmail.com
Wakala wa Usalama wa Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imesema itashirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kama mabalozi wa kutoa Elimu ya usalama wa afya mahala pa kazi na kuwafikia wafanyakazi na jamii kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Hadija Mwenda wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wanachama wa JOWUTA yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusu usalama mahala pa kazi.
Mtandaji Mkuu alisema katika tathmini waliyoifanya wamegundua kuwa bado kuna uelewa mdogo kwa wadau juu ya kazi zinazofanywa na Osha na kwamba ili kukuza uelewa huo wanapaswa kushirikiana na waandishi wa habari.
“Nimejipanga kuhakikisha elimu ya masuala ya afya mahala pa kazi inatolewa kwa asilimia kubwa na ninyi ni, mabalozi wetu kupitia kalamu yenu Elimu itawafikia wananchi hasa wafanyakazi na wataelewa kwa undani zaidi kuhusu usalama wa afya zao mahala pa kazi.
“Nafahamu ninyi ni kundi muhimu na ndio macho na masikio ya wananchi, ili tuendelee kupata taarifa nzuri lazima muwe salama nah ii ni sababu tukasema jukumu letu tuwapatie elimu ili mkaitoe kwa jamii yetu inayotuzunguka,” alisema Mwenda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa JOWUTA, Mussa Juma amesema wanatambua kuwa waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto nyingi katika maeneo yao ya kazi hivyo mafunzo haMwenyekiti wa JOWUTA, Mussa Juma alisema, waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto nyingi katika maeneo yao ya kazi hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kupata uelewa na kuwa mabalozi wazuri.
“Tunafahamu kuwa mafunzo haya ni muhimu kwa waandishi wa habari na tunaimani kuwa ushirikiano huu tuliouanzisha na OSHA utadumu na tutaweza kuwafikia wengine zaidi nchini,” alisema Musa.
Naye Katibu Mkuu wa JOWUTA, Suleiman Msuya alisema chama hicho kinafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na kwa sasa kina jumla ya wanachama 400 nchi nzima na kwamba maombi yao kwa OSHA ni kuendelea kutoa mafunzo hayo kwa wanachama wao wengine waliopo mikoani.
“Dar es Salaam tuna wanachama zaidi ya 80 lakini tuliona katika mafunzo hayo tuwe na washiriki 50 kutoka Dar es Salam na Pwani.
Tunaamini mafunzo haya ni muhimu kwa waaandishi kupitia elimu watakaoipata watakuwa mabalozi wazuri kwa jamii hasa kutangaza kazi zinazofanywa na OSHA.
“Tunawashukuru OSHA kwa kutoa mafunzo haya, tunawaomba mkienda kufanya operesheni zenu tushirikisheni ili umma utambue mnachokifanya,”alisema
0 Comments