Header Ads Widget

DCP MATEI AHIMIZA WELEDI KWA MAAFISA WA POLISI, AGUSIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

 


NA JOSEA SINKALA, SONGWE.


Mkuu wa Kitengo cha kampuni binafsi za ulinzi na Polisi wasaidizi kutoka makao makuu ya jeshi la polisi Dodoma kamisheni ya polisi jamii Naibu kamishna wa Polisi DCP Ulrich Matei, amewataka maafisa wa Polisi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu kwenye kazi zao za kulinda raia na mali zao ikiwa ni pamoja maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kuhakikisha unafanyika kwa amani na utulivu.



DCP Matei angali akiambatana na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Paul Sanga kutoka Kamisheni ya Operesheni na Mafunzo, kwa pamoja wawili hao wamefanya ziara ya kikazi Mkoani Songwe zaidi wakitoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo maandalizi ya uchaguzi. 



DCP Matei amewaelekeza askari polisi kutambua na kuzingatia wajibu wao katika uchaguzi na kutojihusisha na itikadi za kisiasa badala yake wasalie kwenye wajibu wao kwa mujibu wa katiba na sheria zinazowaongoza.



Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kutenda haki bila kujali itikadi za vyama vya kisiasa, dini, jinsi wala kabila na kufanya Taifa kuendelea kuwa la umoja, mshkamano na utulivu kwa maendeleo endelevu.



Kikoa hicho kimefanyika katika ukumbi wa Polisi Vwawa Wilayani Mbozi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya uhamiaji na Jeshi la Akiba (Mgambo) walioungana pamoja na jeshi la Polisi mkoa wa Songwe katika kuimarisha umoja, usalama na uwajibikaji wa pamoja mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI