Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza na viongozi wengine mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya Mhe. Mwalingo Kisemba, wakiwa katika kijiji cha Darajani kata ya Inyala kwenye mradi wa daraja ambalo ijumaa hii (Agosti 30, 2024) linatarajiwa kuwekwa jiwe la msingi na mwenge wa uhuru 2024 baada ya kujengwa na TARURA limegharimu zaidi ya shilingi milion 100.
Daraja hilo linaarifiwa kuua watu watatu hapo awali hivyo kujengwa kwa daraja hilo kwenye barabara ya Imezu Darajani mjini, kunasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa kata hiyo na kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni "Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu".
0 Comments