Na Pamela Mollel,Arusha
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL,CPA Moreni Marwa amesema Shirika hilo kupitia mkongo wa Taifa umeweza kuunganisha Tanzania na Nchi zingine zinazoizunguka katika sekta ya mawasiliano
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha CPA Marwa anasema nchi hizo ni pamoja na Kenya,Rwanda,Burundi,Zambia,Malawi,Uganda na Msumbiji
"Tanzania inajografia nzuri sana hivyo inatoa fursa za nchi zingine kupata mawasiliano kwa urahisi "anasema CPA Marwa
Pia amesema shirika hilo limewezesha baadhi ya makampuni ya simu kupitia mkongo wa Taifa kutoa huduma kwa wateja wao
Aidha ameongeza kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha utoaji wa huduma kidijitali ili kuongeza tija katika Taifa
Katika kuhakikisha shirika hilo linawafikia wananchi kwa ukaribu zaidi imeanzisha huduma ya Faiba mlangoni ambayo inawapa fursa ya kupata intaneti na mawasiliano kwa wakati
0 Comments