Header Ads Widget

MASHINDANO YA BUNIFU ZA KISAYANSI YAFANYIKA LINDI, VIJANA WAHASWA KUTOKATA TAMAA

 




NA HADIJA OMARY 

LINDI

Katika kuhakikisha wanafunzi katika shule za sekondari nchini wanaongeza hari na kukuza bunifu mbali mbali kupitia masomo ya sayansi Taasisi ya wanasansi chipukizi Tanzania (YST) imendesha mashindano mkoani Lindi ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kitaalam wa kubuni na tafiti za kisayansi zenye kuleta tija kwa jamii.

Hatua hiyo inakuja kufuatia kuwapo kwa mwamkoa mdogo wa wanafunzi katika kuyapenda masomo ya sayansi nchini ambapo inaelezwa mpango wa kuwajengea uwezo wanafunzi katika masomo ya sayansi umekua ukitekelezwa toka mwaka 2011 na Tasisi ya wanasayansi chipukizi (YST) ambapo hadi sasa umeonekana kuanza kuleta Matunda

Katika maonesho hayo ya tatu kufanyika Katika Mkoa huo  Jumla ya shule 12 Kutoka Katika shule za sekondari za  zilishiriki  huku  miradi  15 ya kazi za sayansi na teknolojia zimetengenezwa na vijana  hao wanasayasi chipukizi .

Akizungumza wakati wa maonesho hayo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt kheri Kagya kwa niaba ya katibu tawala wa Mkoa huo  wamehasa vijana hao kutokata tamaa Katika Tafiti wanazozifanya.

amesema kuwa  kutokana na gunduzi na Tafiti mbali mbali zinazotokana na uwepo wa sayansi na Teknolojia kwa kiasi kikubwa zimeweza kurahisisha Maisha katika Dunia na ulimwengu kwa ujumla hivyo ili kufikia malengo ya Tafiti wanazozifanya hawatakiwi kukata tamaa.

Akizungumzia maonyesho hayo ambayo yamefadhiliwa na kampuni ya Shell Tanzania Muanzilishi mwenza wa Taasisi ya wanasayansi Chipukizi YOUNG SCIENTISTS TANZANIA (YST) Gozibert Kamugisha amesema wanachokifanya vijana hao ni kutumia masomo ya sayansi wanayoyafanya Darasani na kuyaweka katika vitendo zaidi ili kutumia katika jamii na kuleta manufaa.

"YST ni jukwaa ambalo linajitahidi kujenga utamaduni kwa vijana kwa kufanya utafiti na kugundua vitu vipya kiasi kwamba Hata wanavyoendelea kukua na kuendelea na masomo Yao utafiti uwe ni swala la kiutamaduni na lisiwe swala la kuelekezwa." alieleza Kamugisha 

Amesema lengo la kuyafanyia hayo yote ni kutengeneza kizazi ambacho kinaweza kuchukua jukumu la moja kwa moja kumaliza matatizo yanayowakabili Watu kuliko kusubiri Serikali ama wafadhiri kwa ajili ya kutatua matatizo hayo.

Naye mshauri Mkuu wa maswala ya kijamii kutoka kampuni ya shell Msomis Mmbena Amesema yangu mwaka 2013 kampuni hiyo ilipoanza  kusaidia Mradi wa wanasayasi chipukizi Tanzania na kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa.

" Tumeweza kuona mafanikio mkubwa ambapo wanafunzi wameanza kuendelea kukuwa mwaka baada ya mwaka na niseme tu kuwa tumefarijika kuona shule zilizoshiriki pia zimeongezeka tangu mwaka 2013 huku Afisa Elimu taaluma mwalimu kulwa akieleza namna program hiyo ulivyokuwa chachu ya wanafunzi ndani ya mkoa huo kupenda masomo ya sayansi.

kukamlilika kwa mashindano hayo kwa Ngazi ya Mkoa ndio  Maandalizi ya mashindano ya Ngazi ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika hapo septemba 19 mwaka huu huko jijini Dar es salaam ambapo kwa mkoa wa Lindi Jumla ya shule tatu zitashiriki ambazi ni pamoja na shule ya sekondari Kibutuka iliyoshika nafasi ya Kwanza , shule ya sekondari Nachingwea nafasi ya pili na shule ya sekondari angaza iliyoshika nafasi ya tatu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI