Header Ads Widget

SERIKALI YATOA MIL.900 KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA AKINA MAMA.

 











Na Ibrahim Yassin.Songwe. 

Kutokana na uwepo wa uhaba wa baadhi ya maje ngo ikiwemo la mama na mtoto hospitali ya wilay a ya Mbozi mkoani Songwe hatimaye serikali imet oa Tsh.Milioni 900 kujenga jengo jipya kumaliza tatizo hilio.

Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ni moja ya halm ash kongwe nchini lakini imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa.baadhi ya majengo katika hospitali hiyo hali iliyolazImu akina mama kubanana wakis ubiri huduma.

Wananchi wakiwemo mama wajawazito wame ipongeza serikali kwa ujio wa fedha hzo wakis ema itawaondolea kadhia ya kubanana kutokana na ufinyu wa jengo huku wengine wakiongelea kutozwa fedha.

Stija Sande mjamzito aliyekuwepo hospitalini hapo alisema licha ya uwepo wa sera ya nchi kuwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka 5 kutibiwa bure lakini wamekuwa wakiambiwa wakanunue dawa.

Alisema wananchi wengi wamekuwa na bima ya 30.000 lakini wakifika hospiyalini wanapewa daw a za bei ya chini dawa za bei ya juu wanaambiwa wakanunue nadukani hali inayosababisha wengi kutokata bima.

Matha Mtafya mjamzito alisema amepata taarifa ujio wa fedha hizo anaomba ujenzi ukamilike hara ka ili wahepuke kubanana kwenye jengo hilo kwa ni idadi ya wajaeazito ni wengi ukilinganisha na jengo.

Mganga mfawidhi wa hospitalii hiyo Dkt,Kelvin Masea alisema kitendo cha wajawazito na watoto chini ya miaka 5 kutozwa fedha hakitakiwi kama kuna mtumishi alitoza fedha alifanya makosa.

Kuhusu uchakavu na ufinyu jengo la mama na mt oto alisema serikali imetoa Milioni 900 kujenga jengo jipya hivyo kukamilika kwa jengo hilo kutao ndoa shida hiyo..

Katibu wa umoja wa wanawake ccm wilayani Mbo zi Jenny Chaula lisema wamefika hospitalini hapo waki wa na mbunge kuona ujenzi na kutoa zawadi kwa mama wajawazito hivyo.anaamini matatizo yaliyokuwep o mwanzo sasa hayapo.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Songwe. Emiliana Mwakyoma alisema wanachoongea wananchi ni kweli kwani wamefan ya ziara hospitalini hapo mara kadhaa na kubaini changamoto hizo.

Mbunge wa viti maalum mkoani Songwe (CCM) Juliana Shonza alisema hata yeye akiwa na viong ozi wa chama alishiriki ziara hospitalini hapo na kujionea changsmoto ikiwemo wajawazito na watoto chini ya miaka 5 kutozwa fedha.

Alisema baada ya kubaini hilo walimueleza waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambae nae alimtuma naibu wake hapa na baadae watumishi wengi walihamishwa na kwamba kwa sasa anaamini changamoto hiyo imepungua.

"Sera ya serikali ni mjamzito na mtoto chini ya miaka 5 atibiwe bure kama kuna baadhi ya madak tari wanatoza fedha hilo halikubatiki ,katika vikao vyenu zungumzieni hili sawa Mfawidhi"alisema Shonza.

Shonza akiwa na viongozi wa chama wanawake walifika hospitalini hapo leo Julai 22 kuona ujenzi jengo la mama na mtoto na kupata nafasi ya kuzu ngumza na wagonjwa na madaktari.

""Rais Dkt Samia Suluhu anatupenda wananchi wake ndiyo mana ametupa Milioni 900 kujenga jengo la kisasa la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti, mimi leo nimeleta misaada kuunga jitihada hizo"alisema. Shonza.

Baada ya ukaguzi wa jengo hilo, mbunge Shonza aligawa misaada ya mashuka, vyandarua ,Sabuni, Kanga,Madishi na Pampasi kwa akina mama waja wazito zenye thamani ya zaidi ya Milioni 3.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI