Na Ibrahim Yassn Kyela.
WAVUVI na wafanyanbiashara ziwa Nyasa mwalo wa Kafyofyo uliopo kijiji cha Njisi kata ya Kajunju mele wilayani Kyela mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwatatulia kero sugu ikiwemo kuwajen gea banda la majokofu kuuza vipato vyao.
Mwalo wa Kafyofyo ni kitega uchumi kikubwa cha mapato ya halmashauri huku vijana wengi wakipa ta ajira ya uvuvi na wengine wakiacha kukaa vijiw eni wakianzisha biashara ya samaki na kujiingizia vipato.
Kikwazo kikubwa cha kukwamisha jitihada hizo ni ukosefu wa miundombinu rafiki ikiwemo ukosefu wa barabara ,banda la kupumzikia na la kuhifad hia samaki,umeme na vyoo.
Mwalo huo wa Kafyofyo ni chanzo kikubwa cha mapato ya halmashauri inayodaiwa kuwa na wav uvi na wamliki wa vyombo vya uvuvi na nyavu 500 wanunuzi wakiwa 2500.
Katika Mwalo huo wenye wavuvi na wanunuzi zaidi ya 3.000 wamekumbwa na changamoto hizo na wapo hatar ini kukumbwa na magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na kipindupindu.
Peter Mwantimwa ni mfanyabiashara katika mw alo huo,.alisema licha ya kutoa ushuru wamekuw a wakipigwa na jua na msimu wa mvua inawaishi a kutokana na ukosefu wa banda la kupumzikia.
Mara Jumanne mnunuzi.wa samaki alisema pindi wafikapo Mwaloni wakiwa wanasubiri wavuvi wat oke majini hawana pahala pa kuoumzikia kutokan a na ukosefuwa banda na hata wakipatwa na haja inawalazimu waende vichakani kwenye matete kujisitili.
"Mara nyingi mvua ikinyesha au jua likiwa kali tunakimbilia kwenye nyumba za watu zilizopo karibu na ziwa hilo mara nyingi tulikuwa tunaji hidadhi na hata kujisaidia kwenye vyoo vyao ,kwa sasa wanafunga milango tunakosa pa kwenda "alisema.
Oscar Mwamakula mnunuzi alisema wamelala mika miaka mingi, viongozi wa wilaya,mkoa na Taifa wamefika hapa wamesikia kero lakini hak una walichokifanya zaidi ya kuona ujenzi wa ban da ukianza na kuishia njiani.
Mboka Mwankosole mnunuzi alisema mwaka jana halmashauri ilianza ujenzi wa banda lenye uwezo wa kuhifadhi watu 50 kwa Milioni 6 wakati wao wapo 3.000 na kibaya zaidi ujenzi umekwa ma ukiwa asilimia 10.
Benard Razaro mvuvi wakati serikali ikianza uta tuzi wa kero waanze na vyoo ili watunze mazingi ra kwani kitendo cha kujisaidia vichakani na kwe nye maji au mchangani ni hatari.
Juma Mwaipopo mwenyekiti wa wamiliki na wat umia vyombo vya uvuvi majini alisema wanalazi mika kuuza samak ikwa bei ya nyanya wakihof ia kuharibika kutokana na ukosefu wa banda la maj okofu.
Alisema ombi lao wavutiwe umeme, wajengewe banda la kupumzikia ,banda la majokofu ili sama ki wakibaki waweze kuwahifadhi ili wauzwe kesho yake wakifanyiwa hivyo watakuza kipato mara dufu.
Said Mwamambi Katibu wa mwalo huo alisema malalamiko ya watu hao yanamashiko wani wan alipa ushuru na tozo za nyavu na gara wanunuzi wanatozwa Tsh 500 kwa ndoo ya kilo 20 ya dagaa na ngelwa lakini hakuna huduma inayofanyika katika mwalo huo.
Alisema siku samaki wakikamatwa kwa wingi fedha inayokusanywa kwa ajiri ya ushuru kwa siku inafika hadi laki 5 na kwamba wanaomba sehemu ya ushur na tozo hizo zirudi forodhani kuondoa changamoto zilizopo katika Mwalo huo.
Tangulini Mwambopo mtoza.ushuru wa halma shauri ,alisema inampa ugumu kukusanya ushuru kutokana na wengi wao kugoma kutoa kutokana na kuwa hakuna huduma walizo wekewa katika mwalo huo huku barabara ikiwa mbovu wanapita njia ya mzunguko kwenda mjini.
Ally Mlaghila Jumbe Mbunge Jimbo la Kyela alise ma ni kweli hali ipo hivyo na kuwa atazungumza na mkurugenzi wa halmashauri kuona namna ya kutatua changamoto hizo.
Katule kingamkono Mwenyekiti wa halmashaur i ya wilaya ya hiyo licha ya kukiri uwepo wa chan gamoto hizo alisema wapo kwenye mikakati ya kuweka miundombinu rafiki eneo hilo. Ikiwemo kujenga vyoo vingine vya kisasa .
"Ni kweli kuna umuhimu wa kujenga banda la kup umzikia, Banda la majiokofu kutunzia samaki laki ni sina jibu la moja kwa moja tutakaa vikao na mk urugenzi kuona namna ya kutatua"alisema Kinga mkono.
Mwisho..
Wavuvi na wanunuzi wa samaki Mwalo wa Kafyofyo ziwa nyasa Kyela wakiwa kwenye pilika pilika za kuuza na kununua samaki..picha na Ibrahim Yassin.
0 Comments