Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP - Mufindi.
MADIWANI Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,wameamua kutema cheche kwa Wananchi kunadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Madiwani hao walipata fursa ya kusoma utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Wananchi mbele ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi wakiongozwa na Katibu Siasa na Uenezi Wilaya Ndg.Dikicson Lutevele (Villa) kwenye ziara yake ya kuzungumza na kueleza mafanikio na miradi ya Maendeleo iliyotolewa na Serikali ya CCM.
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi Ndg.Dickison Lutevele Villa aliwaambia Wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kinyanambo A Jimbo la Mafinga kuwa Serikali inatekekeza wajibu wake kwa Wananchi.
" Wananchi CCM inawaomba muendelee kutuamini kwani DKT Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi sana za Miradi ya Maendeleo kwa Wananchi kila Kata" Alisema Villa.
Wananchi wametakiwa kutambua jitihada na Juhudi za DKT Samia anazo zifanya kwa kuelekeza fedha za Maendeleo bila kubagua.
" Ndugu zangu tukumbuke kuwa Maendeleo hayana Chama na kama ni Siasa tujikite zaidi kwenye kujenga hoja mazukwaani na siyo kutumia lugha za kuudhi." Aliongeza .
Aliwaomba Wana Mufindi kutambua Uwajibikaji wa DKT Samia Suluhu Hassan Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa Wananchi na kuwa na maneno ya hekima.
Watanzania ikumbukwe kuwa tunaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024 ni vema kila mmoja ajikite mawazo yake .
" Hivi hii miradi ya Maendeleo kwenye sekta za Elimu,Maji ,Afya na Miundo mbinu ya barabara inayotekelzwa inatokewa kwa kuelekeza CCM peke yake au Wapinzani wa CCM nao ni wanufaika ? Alihoji Villa.
Aliwataka Wananchi kuamini kuwa wote ni Wanufaika maana kama ni huduma za kijamii ikiwepo Afya, Maji, Elimu na Miundo mbinu ya barabara na Nishati Serikali ya CCM haibagui.
Pamoja na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024, lakini aliwaomba Viongozi wa Siasa na Dini kukemea vikali matukio na vitendo vya Ushoga, Ulawiti , Ubajaji na Mauaji ya Albino,Wazee na Watoto .
Hivi hao wanao wadanganya Watu kufanya matukio wao wakifanyiwa hivyo watajisikiaje na hasa familia zao? Alihoji Villa.
"Natoa wito kwa kila mmoja wetu awe mlinzi kwa mwingine na tuhakikishe tunawafichia ili Sheria isheke mkondo wake maana hawa Wahalifu tunaishi nao tusiwafiche"
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.Regnant Kivinge alisema katika Kata yake ya Kinyanambo Wana CCM hawana deni na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe.DKT Samia Suluhu Hassan kwani amegusa kila sekta.
Mhe.Kivinge alisema CCM inawashangaa wanaobeza Juhudi za DKT . Samia ili hali na wao ni wanufaika maana ni sehemu ya Watanzania.
Diwani wa Kata ya Boma Mhe.Julist Paulo Kisoma kwa upande wake aliwataka Wananchi wa Vyama vingine kuheshimu Viongozi waliopo Madarakani badala ya kuwa wazunguzaji wasio na mipaka.
Mhe.Kisema alisema Kata ya Boma yeye ni shahidi kuhusu Miradi ya Maendeleo iliyopokelewa ,hivyo sio vizuri kuibeza muhimu kwa kipindi hiki kuelekeza mawazo na akili zetu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024.
Mhe.Mainesy Kiwelo upande wake aliwaomba Wana CCM kuitunza amani iliyopo na iliyoasisiwa na Rais wa kwanza Hayati Julius Kambarage Nyerere na Waliomfuatia hadi kwa DKT .Samia .
Bi.Kiwelo alisema aliwaomba Wana Mufindi na Watanzania kwa ujumla wao kuilinda amani na kukemea vitendo vyote visivyo vya kimaadili kwa Wananchi.
............Mwisho..........
0 Comments