BAADA ya Mchungaji Peter Msigwa kuondoka ndani ya chadema na kujiunga CCM Siri imevuja kuwa mambo ndani ya Chama hicho Jimbo la Iringa mjini si shwari waraka ulionaswa na Matukio Daima media unaeleza Kila kitu .
Waraka huo huu hapa chini ambao umesambaa kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.
VITA HII NI VITA MPYA YA NANI ATA RITHI UBUNGE IRINGA MJINI
Na vita hii tayari imeanza kwa speed kali na wanao tajwa kumendea nafasi hyo 2025 ni hawa wafuatao
1.ALEX KIMBE
2.FRANK NYALUSI
3.PATRICK SOSOPI
4.LEONCE MARTO
5.PALLAIGA ANDREW
KATI YA HAWA kuna mmoja ameanza kampeni mapema na kampeni yake ni kumchafulia jina mwenzake na hapa ndio utaona VITA INAANZA KUNUKIA
FRANK NYALUSI kupitia ziara yake kwenye kata mbalimbali za iringa mjini amekuwa akimsema vibaya mno ALEX KIMBE amekuwa akimchafua na kumharibia jina kwa kuamini itakuwa ndio nafasi yake kuwa mgombea 2025
Ukifuatilia muendelezo wa ziara zake amekuwa akimshutumu KIMBE kwamba ndio sababu ya MSIGWA kwenda CCM akidhani kuna mtu ana umia kwa Msigwa kuondoka pia amekuwa akimshutumu KIMBE kwamba alipo kuwa MEYA alimpa yeye KAMATI YA UKIMWI tuhuma ambazo ni za uongo na kizandiki kbsaa
HALI HII ya kuchafuana kwa tuhuma za uongo za kuokoteza ni utamaduni mpya kwenye chama chetu hatukuzoe huu utaratibu wa kutafuta madaraka kwa kuchafuana
NAMSHAURI NYARUSI akazane kujenga chama hizi siasa za majitaka aachane nazo mara moja hazita msaidia chochote zaidi ya kuharibu chama na akumbuke nae ana MAOVU MAZITO ambayo kama KIMBE akiamua kuweka wazi pata chimbika namsihi AACHE MARA MOJA.
NAWASHAURI WANA IRINGA..Tuwe wakali dhidi ya huyu Nyalusi na yeyote atakae jiingiza kwenye siasa za hovyo hovyo za kuchafuana hii itakuwa ndio salama ya chama chetu kuepuka mpasuko usio wa lazima
MUDA UKIFIKA kila kitu kitajieleza ni wanachama watakao amua nani awe mbunge kwa sasa tuelekeze nguvu kujenga chama na kujiandaa na uchaguzi ulio mbele yetu
ASANTENI
0 Comments