Header Ads Widget

HISTORIA YAANDIKWA KITABU CHA UTENGEMANO WA AFRIKA CHAZINDULIWA GHANA

Kitabu cha Matarajio ya Utengamano wa Afrika, Mgogoro wa Sahara kilichoandika wanahistoria wawili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaa (UDSM), kimeendelea kusambazwa katika nchi mbalimbali za Afrika baada ya uzinduzi mwingine kufanyika Chuo Kikuu cha Ghana (UG).


Kitabu hicho kilicho chapishwa na African Proper Education Network (APE) kilizinduliwa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha (RUCU) Mkoani Iringa na baadae kikapelekwa Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, Chuo Kikuu cha Johannesburg nchini Afrika Kusini kabla ya Ghana ambako kimezinduliwa jana, Julai 16, 2024.



Mhadhiri wa UDSM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Historia Tanzania Dk Chuhila amesema matarajio yao ni kuona vyuo vikuu mbalimbali Afrika vinajadili kuhusu utengamano wa Afrika, hasa Mgogoro wa Sahara ambao umedumu kwa muda mrefu.

Amesema kitabu hicho kimekuwa kikipokelewa na idara za historian a Sayansi za Jamii kwenye vyuo hicho kutokana na kubeba ujumbe unaohusu Utengamano wa Afrika, baada ya kufanya tafiti za kina nchini Morocco hasa miji ya Layoune na Dakhala.


Akiwakaribisha wanahistoria hao, Mhadhiri wa GU, Dk Aidoo Kojo Opoku amesema kitabu hicho kitakuwa miongoni mwa vile vitakavyotumika kufundishia na kuibua mijadala kuhusu utengamano wa Afrika hasa mgogoro wa Sahara.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI