MHANDISI CHIONDA KAWAWA - MKURUGENZI NACHINGWEA
Na, Matukio Daima App Lindi
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa amepiga marufuku viongozi kuwakandamiza wafanyakazi wa chini wanawaongoza.
Akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa idara ya afya, mkurugezi huyo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakuu wa idara kutumia madaraka yake kuwanyanyasa watumishi wa chini.
Mhandisi Kawawa alisema kuwa kila mfanyakazi ameanzia kufanya kazi ngazi ya chini hivyo ni vizuri kuwajengea uwezo wafanyakazi wenzenu ili waje kuwa wafanyakazi bora kama ambavyo nyie viongozi malipo.
Mhandisi Kawawa amewasihi watumishi kuzingatia maadili ya kazi na kudumisha ushirikiano na upendo miongoni mwao ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi pia amewataka viongozi kuacha tabia ya kunyanyasa wafanyakazi wa chini yao na badala yake kusimamia haki na usawa katika mazingira ya kazi.
Aidha, Mhandisi Kawawa amewasisitiza watumishi hao umuhimu wa kufanya shughuli binafsi za maendeleo ili kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo kwani Wilaya ya Nachingwea kwa miaka mitano baadae itakuwa na uchumi wa madini na itatengeneza fursa nyingi.
Kwa kuzingatia maagizo hayo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nachingwea Dokta Ramadhan Mahiga kwa niaba ya watumishi ameahidi kuboresha ushirikiano baina ya uongozi na watumishi wao.
Hii ni hatua muhimu katika juhudi za Halmashauri ya Nachingwea katika kuboresha huduma na kuhakikisha mazingira bora ya kazi kwa watumishi wake.






0 Comments