Header Ads Widget

CHADEMA NYASA YATUMA UJUMBE SERIKALI ZA MITAA MOMBA, YAWAVUNA 100 KUTOKA CCM.

 






NA JOSEA SINKALA, MOMBA SONGWE.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huko wilayani Momba mkoani Songwe mpakani mwa Tanzania na Zambia, kimeendelea na mikutano yake ya hadhara na kuzungumza na wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa baadaye mwaka huu ili kuwaandaa wananchi na chaguzi hizo za usoni.


CHADEMA kinaendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili kuchagua viongozi bora.


Akizungumza na wananchi hao, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Frank George Mwakajoka, amesema wamejipanga kushinda kwa kishindo uchaguzi ujao ili wananchi wa kata ya Kamsamba na bonde la Kamsamba pamoja na Wilaya nzima ya Momba kutopata shida hususani katika miundombinu ya barabara, maji na huduma za afya.


Pamoja na hayo, Mwakajoka amesema miundombinu ya barabara na maji ndiyo imekuwa kero kubwa kwa wakazi hao hali inayohatarisha usalama wao hasa katika usafirishaji wa mazao na bidhaa mbalimbali za biashara.


Kwa upande wake Gideon Siame ambaye ni Katibu wa CHADEMA wilaya ya Momba na mtia nia ya ubunge jimbo la Momba (CHADEMA 2025), angali akizungumza na wananchi wa Kamsamba amesema CHADEMA itahakikisha inaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujiandikisha huku akionya Chama tawala kwa sasa (CCM) kutowarubuni wananchi na wananchi kutopoteza viongozi wa kweli kwa kurubuniwa na fedha au chochote.


Baada ya mkutano huo kumalizika CHADEMA wamewapokea wanachama wapya 100 ambao wamejiunga na Chama hicho kutoka Chama Cha Mapinduzi CCM.


Siame amewapongeza wanachama hao wapya kutoka CCM na kuwasihi kuungana kwa dhamiri zao na timu ya CHADEMA anayosema ni timu imara na jeshi la ushindi na ukombozi wa Tanzania mara ya pili ili kuleta maendeleo ya kweli.


Mtia nia huyo wa ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani, amesema jimbo la Momba wananchi wake wnaendelea kuwa katika lindi la ufukara licha ya kuwa na raslimali lukuki na kuhangaika na adha ya maji licha ya kupakana na ziwa kubwa na Rukwa lakini bado wananchi wanakosa huduma ya maji safi.


Hivi karibuni Mbunge wa jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe (Namundi) alionekana akiwapokea wanachama zaidi ya mia moja kutoka CHADEMA kwenda CCM na sasa CHADEMA inatangaza kuwapokea wanachama mia moja kutoka CCM.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI