NA WILLIUM PAUL, SAME.
WANANCHI wa kata ya Maore wilayani Same mkoani Kilimanjaro wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mashuka katika zahanati ya Maore ambapo walidai kuwa mashuka hayo yamekuja wakati muafaka kwani walikuwa na uhitaji wa mashuka.
Kauli hizo zimekuja baada ya Mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri kufika katika zahanati hiyo kukabidhi mashuka yaliyotolewa na Rais Samia na kisha kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
Zuena alisema kuwa, katika miaka mitatu ya Rais Samia amefanya mambo mengi makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya.
Alisema kuwa, kwa sasa vifaa tiba pamoja na dawa vimesambazwa katika maeneo mbalimbali kuanzia ngazi za zahanati na kuwataka wananchi kuhakikisha vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mbunge huyo aliwataka wananchi wa kata ya Maore kumlipa Rais Samia kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
"Wapo watu wanapita na helikopta angani na kuwatimulia vumbi sasa jiulizeni matatizo yenu yapo uko juu au yapo huku chini Chama kitachoweza kuwaletea maendeleo na kumaliza matatizo yenu ni Chama cha Mapinduzi hivi vingine vinawadanganya" Alisema Zuena.











0 Comments