Header Ads Widget

MBUNGE NJEZA AENDELEA KUCHANJA MBUGA JIMBONI, MAKUBWA YAELEZWA

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi wake ili kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.


Mbunge Oran Njeza ametembelea na kukutana na wananchi wa vijiji vya Pashungu na Iwowo kata ya Itawa Umalila tarafa ya Isangati ambapo ameeleza mambo mbalimbali yaliyotekelezwa.


Mbunge huyo anaendelea kusikiliza kero za wananchi na kueleza utatuzi wake na mambo mengine lukuki ambayo yametekelezwa na Serikali ya awamu ya sita hasa usambazaji wa umeme hadi vijijini na sasa unaelezwa kwamba utakwenda vitongojini (ujazilizo), usambazaji huduma ya maji, ujenzi wa barabara na madaraja ili kuwasaidia wananchi hususani wakulima vijijini.



Akiwa katika kijiji cha Pashungu na baadaye Iwowo Mbunge Njeza amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo ambapo miradi mbalimbali imeendelea kujengwa na kuahidi kuendelea kuikumbusha Serikali kutekeleza wajibu wake kuhakikisha wananchi wanaishi kwenye mazingira bora kwa maendeleo endelevu.


Amesema kuhusu zao la Pareto limeshapanda bei kutoka shilingi 1500 miaka kadhaa iliyopita na sasa ni shilingi 3500 kwa kilo moja na kwamba shauku yake ni kuona bei inaendelea kuwa nzuri zaidi na hata kulipwa kwa dola ili kumnufaisha mkulima.


Amesema kuhusu madaraja kwamba Serikali kupitia Wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA wilayani Mbeya imejenga madaraja mengi na machache ambayo bado ameitaka TARURA kuendelea kutatupia jicho la pekee ili kuyaboresha pamoja na barabara.


Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Mbeya Mhandisi Arcad Tesha amepokea kero hizo kuhusu barabara na madaraja na kuahidi kuyaingiza kwenye bajeti ijayo.


Diwani wa kata ya Itawa Mhe. Elia Mwampamba ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi wake ikiwemo umeme ambao ulikuwa ni kitendawili sasa umefika vijiji vyote vinne na sasa utaelekezwa vitongojini, ujenzi wa madaraja na  barabara kwa sehemu na kuomba changamoto ambazo bado zipo niendelee kushughulikiwa hasa uimarishaji miundombinu ya barabara, maji na uanzishaji shule mpya ambayo inajengwa na wananchi kutokana na shule mama ya msingi Iwowo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI