Header Ads Widget

NMB IMEELEKEZA ZAIDI YA BILIONI 20 KATIKA KUJENGA KESHO ILIYO BORA BBT

 



Shilingi tilioni 1.61 zimetolewa mikopo ndani ya miaka sita katika bank ya NMB kwa kuwezesha ufugaji wa samaki na mazao ya chakula nchini 


Akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa Maonyesho Jumuhia ya Wafugaji kibiashara nchini TCCS Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kilimo Isaac Masusu huko Ubena Chalinze mkoani Pwani amesema pia bank hiyo imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 20 ambazo zimeelekezwa katika program ya kujenga kesho iliyobora BBT. 


Masusu amesema NMB inatambua changamoto ya upungufu wa mitaji ambayo hupunguza uzalishaji  wa kisasa wenye tija na ndio maana wamefanya kuwezeshaji huo wa mikopo.


Amefafanua kuwa benki ya NMB imekuwa ndio benki ya kwanza nchini kuanza kutoa mikopo ya riba nafuu na tulitoa zaidi ya bilioni 100 kwa wakati huo na pesa hiyo ilitolewa kwa Wafugaji nchini.


"Lakini pia benki yetu inatoa mafunzo kwa wakulima kupitia taasisi tatu za NMB foundation, mafunzo hayo ni kwa vijana na akina mama pamoja na wafugaji kwenye maeneo yao pasipo gharama yoyote" alisema Masusu 



Awali Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wafugaji wa Kisasa  Tanzania NCCS ,Naweed Mulla amemshukuru Mheshimiwa Rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kutikana na serikali  kuwashika mkono  wafugaji wa kisasa.


Mulla amesema  kuwa maonesho haya yanalenga  kuwanyanyua  wananchi  na wafugaji wa kisasa pamoja na  kuwawekea  mazingira  sahihi huku amesema kuwa  kauli mbiu ya mwaka huu inasema  tufuge kibiashara  tuijenge kesho iliyo bora.


"Mhe.Rais amekua akitupa maneno ya  kututia moyo  pindi awapo katika majukwaa mbalimbali  jambo ambalo linazidi kutuje nga na kutukuza zaidi"amesema Naweed.


Mwenyekiti huyo wa TCCS Naweed amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewapa bajeti mara mbili kwa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi hivyo tunaahidi kutoa  ushirikiano  wa kutoa maoni  yetu  katika sekta hii ya ufugaji wa kisasa na tuna ahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kukuza uchumi wa nchi kupitia ufugaji wa kisasa.


Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti akifungua Maonyesho hayo aliwapongeza Jumuhia ya Wafugaji kibiashara kwa kufanya Maonyesho hayo yanayoonyesha Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara ambao utasaidia kuongea Soko la nyama ya Tanzania Kimataifa.


Tanzania  ni nchi ya pili kwa mifugo barani Afrika pia tuna ng'ombe  zaidi ya Mil.37.


Maonesho  hayo yamefunguliwa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti  yafungwa kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Biteko.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI