Na Hamida Ramadan Matukio Daima App Dodoma
JESHI la Kujenga Taifa JKT limetoa wito wa Kuwaita Vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha sita kwa Mwaka 2024 kutoka Shule Zote Za Tanzania Bara kuhudhuria Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa Mwaka 2024.
Hayo yameelezwa Leo Jijini Dodoma na Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye ni Mkuu wa Utawala Tawi la JKT,wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu wito huo wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria Mwaka 2024 ambao wanatakiwa kuripoti Juni Mosi Mwaka huu.
Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo hayo vijana hao.
Brigedia Mabena amebainisha kuwa JKT linawataka Vijana hao kuripoti wakiwa na Vifaa mbalimbali ikiwemo Shuka za kulalia.
Hata hivyo amesema,orodha kamili ya majina ya Vijana hao na Makambi ya JKT waliypangiwa na maeneo ya makambi hayo yalipo na vifaa wanavyotakiwa kaenda mavyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz
"Tunaishukuru serikali ya awamu ya Sita kwani imeendelea kuboresha makambi na vijana wote watakao wasili hakutokuwa na changamoto yotote , " Amesema Brigedia Jenerali Mabena
Hata hivyo amesema licha ya kufundishwa uzalendo na Ukakamavu lakini pia katika kambi hizo kutakuwepo na mafunzo ya ujasiriamali kama vile kilimo, Ufugaji, Uvuvi na namna ya kutengeneza sabauni za maji na vipande bila kusahau sabauni za usafi majumbani.
" Mafunzo haya yamekuja baada ya kuona sio wote watakaoishia kuwa Wanajeshi la bali wengine waweze kutoka na ujuzi uwasaidie huko watakapokwenda, "Amesema Brigedia Jenerali Mabena
Sambamba na hilo ametoa Tahadhari kwa wazazi na walezi yakwamba mafunzo hayo hayana ada wala Tozo .
" Kipindi kama hiki kunabaadhi ya watu wasiowaaminifu wamekuwa wakitapeli wananchi hivyo niwaombe kuacha vitendo vya kitapeli kwani mafunzo hayo yanatolewa bure, "Amesema Brigedia Jenerali Mabena
Hata hivyo vijana hao wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkomo- Mara, JKT Msange- Tabora, JKT Ruvu- Pwani, JKT Mpwapwa, Makutupora JKT Mgambo na JKT Maramba- Tanga, JKT Makuyuni, Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwe na JKT Mtabila- Kigoma JKT Itaka-Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa- Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi, JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.
0 Comments