Header Ads Widget

TANESCO YAWAPA SOMO WENYEVITI WA MITAA WILAYA YA KINONDONI NA UBUNGO

 


Na Fatma Ally Matukio na Habari App

Shirika la umeme TANESCO  limekutana na wenyeviti wa mitaa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Ubungo lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa watendaji hao kwani shirika hilo asilimia kubwa utendaji unaanzia kwenye mitaa.


Akifungua kikao kazi hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Altbert Chalamila  kilichoandaliwa na TANESCO kwa ajili ya Wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo amesema wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Serikali kwa kuwa miradi hutekelezwa katika maeneo yao.



"Hata miradi mingi ya TANESCO iko kwenye mitaa hivyo, ni imani yangu kuwa kupitia kikao kazi hiki wenyeviti wote wanakwenda kuwa mabalozi wa kueleza huduma nzuri zinazotolewa na TANESCO pia kulinda miundombinu ya Shirika hilo"amesema RC Chalamila.


Aidha ameipongeza TANESCO kwa kuona umuhimu wa kukutana na kundi hilo muhimu ili liweze kufahamu kwa kina majukumu ya shirika hilo lakini pia kutoa mawazo na ushauri wa namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma za nishati ya umeme kwa wananchi hususani katika mitaa yao.



Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bwana Lazaro Twange amesema Shirika hilo kwa kutambua Wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu likaona liandae kikao kazi kwa ajili yao ili kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano .


Aidha, amesema kuwa mfumo huo utatusaidia kujua wananchi wanasemaje kuhusu huduma za TANESCO pia wenyeviti wawe na uwezo wa kuelewa nini kinafanywa na shirika pamoja na kuwaelimisha wananchi walioko katika maeneo yao.


Ameongeza kuwa, utekelezaji wa miradi ya TANESCO uko kwenye ngazi ya mitaa ambayo huongozwa na wenyeviti wa Serikali za Mitaa .



Mkurugenzi Lazaro Twange amemkabidhi RC Chalamila na Viongozi wachache wa Mitaa Jiko la Umeme ambalo linatumia umeme kidogo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya Nishati safi kwa Jamii.


Amesema licha ya kufanya kazi kubwa ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme bado Shirika limejizatiti kuhakikisha huduma bora inawafikia wateja kwa haraka na kwa wakati sahihi, akisisitiza mkutano huo pia umelenga kuwa karibu na wananchi kupitia Wenyeviti hao wa Serikali za Mitaa.



‘’TANESCO tumejitahidi kuwa karibu na wananchi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja, tunamshukuru sana Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Miradi inakamilika na wananchi wanapata umeme wa uhakika. Kazi  yetu ni kuendelea kupanga mikakati ya kuhakikisha wananchi wanaunganishiwa umeme  na kupata huduma bora,’’ liafafanua Twange.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI