Header Ads Widget

MUNGAI ATETEA NAFASI YAKE UENYEKITI CHADEMA MKOA WA IRINGA

 

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa mchungaji Peter Msigwa akiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa Uchaguzi Chadema mkoa wa Iringa wakati Uchaguzi wa Marudio ukifanyika ukumbi wa Kartasi mjini Iringa 


TAZAMA FULL VIDEO HAPA

VIDEO NZIMA BOFYA HAPA


VIDEO ZA VURUGU ZA UCHAGUZI WA NJOMBE BOFYA HAPA


ALICHOKISEMA SUGU BOFYA HAPA


MSIGWA ATOA KAULI HII TAZAMA VIDEO HII

Na, Matukio Daima App Iringa

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendelea (CHADEMA) mkoa wa Iringa William Mungai amefanikiwa kutetea, nafasi yake ya uenyekiti kwa kupata kura 47 huku mpinzani wake Emmanuel Chengula akipata 34.

 

Uchaguzi ulikuwa na wagombea wawili katika nafasi ya uenyekiti mkoa wa Iringa na wapiga kura 81.

 

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, amewashuru wanachama wote waliompigia kura, huku akiwataka wale ambao hawakumpigia kura kuunga naye kwa sasa ili kuweza kujenga chama kwa pamoja huku akiwataka wanachama wa chama hicho kwa sasa kuvunja makundi na kuelekeza nguvu zao katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

 

“Ni washukuru wagombea kwani ukipambana na mtu uwezo wako unaonekana, uwezo umeonekana nusu na nyingine tuna kwenda kuonyesha uko juu kwingine” Alisema Mungai.

 

Mungai pia amewapongeza viongozi wenzake wote ambao nao wamechaguliwa katika uchaguzi wa leo, huku akiwasisitizia uwajibikaji bora pamoja na kuwashawishi wale ambao hawajawapigia kura kwa kushirikiana nao kwani chama hicho ni cha upendo bila uoga.

 

Mgombea Uenyekiti Chadema Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi Sugu akimpongeza mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Wiliam Mungai kwa kutetea nafasi yake 

“Ni matumaini yangu kwa hii timu ninayoiona hapa ilivyo na moyo wa ushindi tuta kwenda kunyakuwa angalia asilimia themanini ya ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji” Alisema Mungai.

 

Naye, Wakili Msomi Emmanuel Chengula amesema anakubaliana na matokeo ya uchaguzi huo kwa kuwa ulikuwa huru ba haki na wenye uwazi kwa wagombea wote, huku akiahidi kuendelea kuwa mwanachama hai wa Chadema kwa kufuata sheria na taratibu za chama hicho kwa kushirikiana na wagombea wenzake ambao wameshinda.

 

“Kura ambazo nimezipata naamini ndizo nilistahili kupata, huwa tunasema safari moja inaanzisha nyingine, kwa hiyo sehemu ambayo nimekosea naamini wakati mwingine nitakapo gombea nitaimarika zaidi”

 

Wakili Chengula, amesema ataendelea kukitumikia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwani bado anaimani na sera zake, na ndiyo chama pekee amewahi kujiunga hivyo kwa sasa kazi kubwa aliyo nayo ni kuungana kwa pamoja ili kuhakikisha chama hicho kinaenda kushika dola.

 

Kwa upande wake aliyekuwa meya wa manispaa ya Iringa mjini na mwanachama wa chadema Alex Kimbe amesema ushindi huo unaakisi matokeo ya uchaguzi wa kanda ya Nyasa ambao unatarajiwa kufanyika mei 29 mwaka huu.

 

“Sisi kama timu Mungai tunajivunia ushindi huu, na sasa kwa matokeo haya tunakwenda kushinda uchaguzi kanda ya nyasa kwa sababu hawa walioshinda ndiyo wapiga kura katika uchaguzi huo” alisema Kimbe.

 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI