Na Pamela Mollel,Arusha
Wito umetolewa kwa wamiliki wa migodi mbalimbali hapa nchini kuagiza bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha Transfoma cha Tanelec kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kuthamini bidhaa za ndani kwa kukuza uchumi
Mtaalamu wa vifaa vya umeme kutoka kiwanda hicho cha Tanelec Joseph Tiba anasema upo umuhimu mkubwa wa migodi hiyo kuagiza bidhaa kiwandani hapo ili kuokoa gharama ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi
Aliyasema hayo wakati Waziri wa Madini Anthony Mavunde alipotembelea banda lao katika mkutano wa jukwaa la tatu la utekelezaji katika sekta ya madini uliofanyika jijini Arusha katika kituo cha mikutano ya kimataifa AICC
Tiba alimueleza Waziri kuwa pamoja na uzalishaji wa vifaa vya umeme katika kiwanda hicho wameweza pia kutoa mafunzo ya mamna ya kufunga mitambo hiyo jambo ambalo limepelekea kupatikana mafundi wengi tofauti na hapo awali walikuwa wakitoka nje ya nchi
Aliongeza kuwa vifaa vya umeme vinavyotengenezwa na kiwanda hicho watumiaji wakubwa ni wamiliki wa migodi
0 Comments