Header Ads Widget

UCHAGUZI WA CHADEMA NJOMBE WAGUBIKWA NA VURUGU, WASIMAMA KWA MUDA.




 NA JOSEA SINKALA, NJOMBE.


Hali ya sintofahamu imeibuka kwenye mkutano wa uchaguzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Njombe baada ya baadhi ya wanachama kutaka wajumbe wa muda kutoka Wilaya ya Makete (Task force) wasipige kura kwenye uchaguzi huo wa marudio.


Baadhi ya wanachama wamesema msimamizi wa Uchaguzi huo Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA (Bara) Benson Singo Kigaila hajatenda haki kusema task force wanaruhusiwa kupiga kura, hii ni baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Rose Mayemba kufungua kikao na baadaye mgombea mwenzake wa uenyekiti Ahadi Mtweve na baadhi ya wajumbe kutaka katiba isomwe ikiwa task force wanapaswa kupiga kura.




Ndipo baadhi ya wajumbe wakaendelea kunyosha mikono wakitaka mwongozo wa msimamizi na kusimama wakitaka katiba ya chama hicho isomwe jambo ambalo halikuwekwa bayana.


Wakizungumza kwenye ukumbi huo wa mkutano baadhi ya wanachama na viongozi ambao ni wajumbe kwenye mkutano huo wamesema hawajaridhika na usimamizi wa uchaguzi huo katika hatua za awali wakidai wajumbe wanaelezwa kuwa tisa kutoka Wilaya ya Makete sio wapiga kura.


Hata hivyo Naibu katibu mkuu wa CHADEMA (Bara) Benson Kigaila amesema viongozi waliowekwa kwa muda baada ya mgombea uenyekiti Ahadi Mtweve kukata rufaa juu ya matokeo yanayodaiwa kuhujumiwa wanapaswa kupiga kura jambo lililosababisha vurugu ukumbini.



Nje ya pazia kinachosikika kutoka kwa baadhi ya viongozi na wana CHADEMA ni kana kwamba viongozi wanaopingwa kupiga kura wanadhaniwa kumwongezea kura Rose John Mayemba kuwa Mwenyekiti huku wengine wakidhani kuwakataza kupiga kura ni kukiuka katiba ambayo inataka viongozi wa muda yaani task force ya nafasi za wajumbe kupiga kura ambapo hata hivyo mkutano huo wa uchaguzi ukalazimika kuahirishwa kwa muda hadi hapo baadaye kwa kadri itakavyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI