Header Ads Widget

OTHMAN MASOUD ATOA KAULI KUFUNGWA KWA UVUVI ZIWA TANGANYIKA

  

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAKAMU wa kwanza wa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othman Masoud Othman ametaka suala la ufungaji shughuli za uvuvi kwenye ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu liangaliwe vizuri ili lisiache athari za kiuchumi kwa wananchi ambao Maisha yao yanategemea shughuli hizo za uvuvi.

 

Masoud alisema hayo alipofanya ziara kutembelea bandari ya Kibirizi mjini Kigoma ambapo alikutana na watu wanaofanya shughuli mbalimbali kwenye ziwa Tanganyika waliomweleza kuwa kufungwa kwa shughuli za uvuvi kutakuwa na athari kubwa kwao kiuchumi.


 

Makamu huyo wa Raisi alisema kuwa anao uzoefu wa Zanzibar ambapo shughuli za uvuvi hazifungwi kote bali baadhi ya maeneo ya mazalia ya Samaki na kuachwa eneo la maji makubwa wavuvi waendelee na shughuli zao bila kuathiri ukuaji wa Samaki na dagaa.

 

Akiwa mkoani Kigoma Makamu huyo wa Raisi wa kwanza wa Zanzibar alisema kuwa amepokea malalamiko mbalimbali kuhusu kufungwa kwa shughuli za uvuvi ziwa Tanganyika na kwamba atafikisha malalamiko hayo kwa maandishi kwa Raisi Samia Suluhu Hassan ili wataalam wachukue hatua za ufungaji huku wakiweka unafuu wa hali za uchumi kwa wananchi waliokuwa wakitemegea uvuvi kama njiia yao kuu ya kuwaingizia kipato.

 


Awali Katibu wa wavuvi katika Mwalo wa Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mohamed Kasambwe alisema kuwa mpango wa kufungwa kwa shughuli za uvuvi ziwa Tanganyika haukuangalia athari ambazo watazipata watu wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi kwa miezi hiyo mitatu.

 

Kasambwe alitoa mfano wa mpango wa ugawaji vizimba vya kufugia Samaki ambao utafanyika Mei 9 mwaka huu wiki moja kabla ya kufungwa kwa shughuli za uvuvi wakati Samaki wanaopaswa kuvunwa watachukua miezi sita hivyo ugawaji huo wa vizimba kwa sasa hauna maana katika kukabili athari za watu wanaofanya shughuli za uvuvi.

 

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI