Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekemea
tabia ya malumbano na kuvutana kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri ya
Jiji la Arusha kwani jambo hilo limesababisha kukwama kwa miradi mingi ya
maendeleo licha ya Serikali kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi hiyo.
Ametoa kauli hiyo leo, mara baada ya kupokea ripoti ya utendaji wa Wilaya ya Arusha, iliyoonyesha kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo kutokana na mabishano, malumbano na kutokuelewana kati ya Menejimenti ya Wilaya, Baraza la madiwani na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa, amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa migongano hiyo ya kutokuelewana kati ya viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kumesababisha adhabu kubwa kwa wananchi kutokana na miradi muhimu kukwama na hivyo kuwachelewesha kimaendeleo.
"Ingekuwa ni mamlaka yangu ningevunja Mamlaka yote ya Jiji la Arusha maana siobi umuhimu wa Jiji kuwepo katika kuwaletea maendeleo wananchi" alisema Makonda.
Kufuatia hali hiyo, Makonda, amelitaka Baraza la
Madiwani Jiji la Arusha kujitafakari na kuamua kuwa sauti ya wananchi
kikamilifu na kupambana kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana kwa
kukamilisha miradi yote ya maendeleo kwa wakati.
0 Comments