Awamu ya kwanza ya mbegu zenye thamani ya shilingi 63,700,000
zimepokelewa Rufiji kutoka kwenye ya ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa kwa ajili ya kusaidia Wananchi ambao mazao yao yalisombwa na maji ya mafuriko ya mto Rufiji hivi karibuni.
Mbegu hizo zimepokelewa katika ghala la Ikwiriri wilayani Rufiji ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mheshimiwa Mchengerwa kutoka katika michango ya milioni 50 alizotoa yeye mwenyewe, Wakuu wa mikoa 26 nchini kutoa michango ya shillingi milioni 44 na shilingi milioni 13.7 kutoka kwa wazawa wa Rufiji wanaoishi nje ya Rufiji na kufanya Jumla ya shillingi milioni 107.7.
Amesema alikabidhiwa na Mheshimiwa Mchengerwa fedha hizo hivyo manunuzi ya mbegu hizo ni sehemu ya fedha kiasi cha shilingi milioni 63.7 ambapo bado kuna Salio la mbegu zingine zenye thamani ya shilingi milioni 43 zitaletwa.
Meja Gowele amesema amepokea mbegu bora hizo za Mahindi kutoka kampuni ya SEEDCO kilo 9,100 sawa na mifuko 4,550 ya kilo mbili.
Usambazaji wa Mbegu hizo kwa awamu ya
kwanza umefanyika ambapo jumla ya kilo 8,984 za mbegu hizo zimesambazwa katika kata za Mwaseni, Kipugira na Ngorongo.
Akizungumzia hali ya usambazaji wa Mbegu hizo Meja Gowele ametoa shukrani za dhati Kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mohamed Mchengerwa kwa kujali na kuthamini Wananchi wake Kwa kuhakikisha anatoa Mbegu Kwa Kila Kaya iliyoathiriwa na mafuriko ambapo Kwa awamu ya kwanza Mbegu hizo zitawasaidia Wananchi kupanda tena mazao mashambani baada ya maji kupungua hali itakayopelekea kurudisha matumaini na kupunguza ukali wa hali ya upungufu wa chakula ambao ungejitokeza baadae.
Aidha amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuimarisha mahusiano Bora na sekta binafsi pamoja na Taasisi mbali mbali ikiwemo Lions Club ambao wameunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mchengerwa Kwa kuongezea Mbegu Ili Wananchi waendelee na shughuli za Kilimo baada ya athari za mafuriko.
Aidha Meja Gowele anaendelea kutoa Wito Kwa Taasisi na mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na Watu binafsi kuendelea kuunga Mkono juhudi za Serikali pamoja na Mbunge wa Jimbo Hilo kuwasaidia Mbegu wananchi hao Ili kurudisha Hali Kilimo kama ilivyokuwa awali.
Katika hatua nyingine,, Taasisi ya Lions Club Foundation imetoa kilo 400 sawa na mifuko 200 ya kilo mbili yenye thamani ya shilingi 2,800,000.
0 Comments