Header Ads Widget

TLS YAWAPIGA MSASA ASASI ZA KIRAIA SHERIA YA UHURU WA KUJIELEZA

Na Hamida Ramadhan, matukio Daima app Dodoma

LICHA ya Tanzania kuwa nchi ya Kidemokrasia lakini imekuwa ikipitia vipindi tofauti tofauti hali inayopelekea wakati wengine haki na Uhuru wa kujieleza kuminywa au kukandimizwa katika jamii. 


Kutokana na hali hiyo Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) wameona  kunahaja ya kuwajengea uwezo na kutafuta namna ya kusaidia serikali na wananchi kwenye masuala yote yanayohusu sheria ili nao wawe na uelewa sahihi juu ya haki zao . 


Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Afisa miradi chama cha Wanasheria Tanzania TLS  Victor Mbulingwe amesema moja ya malengo kuanzishwa kwa chama hicho ni kusaidia serikali na bunge katika Mambo yote yanayohusu sheria au utendaji kazi wa sheria. 

Sisi kama TLS kazi yetu kubwa ni kuhakikisha utekelezaji wa sheria au kwa lugha nyengine utekelezaji kazi sheria unakuwa upo sawa sawa na haki za watu waliopo katika nchi inapatikana, "amesema . 


Na kuongeza "Hivyo basi tumeona ni vyema kuwasaidia au kuwajengea uwezo Asasi za kiria katika masuala ya Uhuru wa kujieleza ambapo Uhuru wa kujieleza unalindwa na Katiba yetu katika kifungu cha kwanza kifungu kidogo cha 18 "abcd", " Amesema Buligwe


Amesema Mtu anaouhuru wa kutoa maoni yake, kupokea taarifa kutafuta taarifa, kusambaza taarifa bila kujali mipaka ya nchi lakini pia kupewa taarifa yoyote katika nchi. 

" Tanganyika law society ili kuweza kuhakikisha jamii tunayoishi nayo tunaipa kile wanachostahiki kukipata tumeona tuwajengee uwezo hawa Asasi za kiria ili nawao waende kutoa elimu katika jamii zao huko chini. 


Lakinipi mafunzo hayo sio kwa Asasi za kiria pekee Bali makundi yote yatafikiwa


Kwa upande wake Rose Ugulumu Kaine Mkurugenzi  sharika la Biashara na haki za Binadamu Tanzania amesema Mafunzo yanayifanyika na TLS yanawasaidia namna bora ya kufanya kazi katika kipengele kizima ya masuala ya haki ya kujieleza katika jamii. 


"Sio Sisi tu watu tunaowafundisha jamii lakini na watu kujua haki zao za kujieleza kwa mba wana haki ya kujieleza kulingana na sheria ambazo kuna kimataifa zinazosimia hiyo haki na kunasheria ya ndani ya nchi ambayo inasimamia haki ya kunieleza ambayo ni Katiba yetu ya nchi, " Amesema. 

Na kuongeza "Hapa leo tunafundishwa jinsi gani ya kujieleza na Mambo mbalimbali tunayofanyia kazi na haki ya kujieleza na sheria hiyo kwa ujumla, " Amesema Kaimu Mkurugenzi huyo


Aidha amesema kuwa,Kujieleza lazima kuwe na mipaka kwani huwezi kujieleza kinyume na sheria kusiguse utu wa mtu hivyo tunafundishwa misingi Bora kusimimia kama watetezi haki za binadamu 


"Tumepewa Uhuru wa kujieleza lakini tuzingatie masuala sheria, masuala ya mahusiano ya kijamii masuala ya Mila na desturi zetu ili tuweze kuleta ule Uhuru wetu uweze kutumika kifasaha na kuleta maendeleo katika jamii yetu, " Amesema Kaimu Mkurugenzi huyo Rose


Naye Omary Lubuva kutoka Shirikisho la watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) mekipongeza chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) kwa kuwajengea uwezo hasa katika sheria ya haki ya kujieleza kwani waliowengi wa Tanzania sio Wanasheria kwa kiasi kikibwa na uelewa wao huu ya kujiekeza sio mkubwa. 

Amesema Kwa kupitia mafunzo hayo yaliowakusanya makundi tofauti tofauti mafunzo yatawasaidia katika kuwafikia wenzawenzao ili kutambua na kuifahamu sheria hiyo ya haki ya kujiekeza. 


Amebainisha kuwa,sheria hiyo ndio inayosaidia kuzifikia au kuzielewa sheria nyingine huku akiwa na uelewa mpana na hatimaye haki kupatika . 


"Tunaimani baada ya hapa na Sisi kama viongozi SHIVYAWATA tutakwenda kuwajengea uwezo ili mwisho wa siku kuweza kudai haki zao na kutumia vizuri maarifa ya sheria ya Uhuru wa kujiekeza," Amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI