Header Ads Widget

ASILIMIA 6 PEKEE YA WANANCHI WA MJI NJOMBE NDIYO WANAOKULA MAYAI




KURUTHUM SADICK MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Ripoti toka ofisi ya Lishe halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe  zimebainisha kuwa ni Asilimia 6 pekee ya wakazi wa Halmashauri hiyo wanao kula mayai huku maziwa wakinywa asilimia 16 hatua inayofifisha jitihada za kupambana na udumavu.


Katika Kongamano la wanawake la kuwajengea uwezo katika kutokomeza udumavu tarafa ya Njombe mjini Ofisa Lishe Halmashauri ya mji wa Njombe bwana  Michael Swai amesema Wananchi wengi hawatumii mayai na maziwa ilihali ni miongoni mwa vyakula muhimu katika kupambana na udumavu.


Awali Lilian Nyemele Ofisa Tarafa ya Njombe mjini amesema wamelazimika kuandaa Kongamano hilo likiwa na lengo la kutoa elimu yan udumavu,Mikopo ya wanawake,vijana na wenye ulemavu pamoja na elimu ya ujasiriamali kwa wanawake.


Kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe,Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick amesema Kongamano hilo litumike kuwaelimisha wanawake ili wakafikishe elimu ya lishe mpaka vijijini ili jamii iondokane na Udumavu kwa watoto.


Baadhi ya akina mama akiwemo Vumilia Bange na Isabela Malangalila  wanakiri kuwa majukumu mengi waliyo nayo yanasababisha kushindwa kutenga muda wa kuwaandalia lishe nzuri watoto wao.


Winfred Kayombo ni baba ambaye anasema suala la Malezi kwa watoto linapaswa kuwa shirikishi kwa Wazazi wote kwani hata wakiacha fedha za matumizi bila usimamizi hakutakuwa na tija.


Mkoa wa Njombe unashika nafasi ya pili Kitaifa kwa udumavu ukiongozwa na mkoa wa Iringa ambapo jitihada mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ikiwemo kuanzisha kampeni maalumu ya Lishe chini ya mkuu wa Mkoa wa Njombe ikienda na Kauli mbiu ya ''Kujaza Tumbo sio Lishe Jali unachokula''.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI