Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU MAFINGA ,WAUNDA KAMATI KWENDA KUMUANGUKIA MKUU WA MKOA WA IRINGA RC PETER SERUKAMBA

 .   


                                  Na Fredrick Siwale -Matukio Daima - APP Mafinga Mufindi.       

        Wakizungumza na Matukio daima APP Wamesema wameunda tume hiyo maalumu ili ifike ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Peter Serukamba kumuomba aingilie kati kutatua mgogoro wa vibanda 331 vya Wafanyabiashara hao.  

   Wakiizungumzia hoja hiyo katika kikao chao cha kawaida katika ofisi za soko kuu Mafinga ,Mjumbe wa mwakilishi wa Vibanda hivyo Bw.Michael Nziku maarufu " My document"alisema wamecikia uamuzi wa kwenda kwa mkuu wa mkoa baada ya kuona Uongozi wa Wilaya umeshindwa kuwasaidia kama Wananchi na badala yake unatumia nguvu kubwa kuwadidimiza na kushindwa kufikia muafaka wa jambo hilo.                                    


  "Sisi lengo letu ni kuhusu vibanda 331 ambavyo vimekuwa kwenye sintofahamu ya muda mrefu na kizungumkuti kwetu kwa sababu kikao chetu tulikuwa tunamhitaji Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mh.Legnant Kivinge ili tuweze kufahamu yale makubaliano yetu ya mkataba wa miaka 14 kwani tulikuwa tunasubiri kwa ajili ya kusaini mikataba hiyo na siyo kubomolewa " Alisema my Document .    

                     Aliongeza kusema kuwa " tumeshangazwa kuona Halmashauri wamepita wakibandika mabango katika vibanda 331 yakiwa na ujumbe usemao kuwa wanatakiwa kubomoa vibanda vyao  na kuacha ardhi ya Serikali vinginevyo vitabomolewa kwa gharama za Wafanyabiashara" Aliongeza kusema. 


               Katika kuendelea kusisitiza alisema wao kama Wananchi na Wafanyabiasha wa chini na wakati katika vibanda hivyo 331 hawana ugomvi na Serikali yao ,bali wanahitaji kufikia makubaliano ya awali ili kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla.        



                Wafanyabiashara wajibu wao wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Halmashauri  ni utaratibu unaotakiwa kutekelezeka ila kinacho washangaza wao ni kuona Watu wachache nasababisha wasiweze kufikia muafaka wa suala hilo .Alimalizia kusema ." My Document .     


                       Mfanyabiashara mwingine wa vibanda hivyo Bi.Heleni Mgeni alisemakuwa Viongozi wa Soko waliwaambia Halmashauri hiyo ilidai kuwa Wafanyabiashara hao wanatakiwa kukubali kuingia mkataba wa miaka 14 na kulipa fedha hizo sh.25,000 kila mwisho wa mwezi .                              


  Hivi tunashangaa kuona mabango ambayo yanatutaka kuvunja vibanda ambavyo tumevinga miaka mingi iliyopita "Alisema Bi Mgeni.      


       Mwenyekiti wa Soko kuu Mafinga ,Philinus Mgaya alisema kuwa vibanda hivyo 331 havikujengwa kwa utaratibu huku changamoto ikiwa ni namna Serikali inavyotaka kuvichukua kwa mabavu vibanda hivyo.                                   


Utaratibu wa kumiliki vibanda hivyo imekuwa changamoto kutoka awali ilipodaiwa kuwa wakate sh.25,000 na sh.25,000 nyingine ilipwe taslimu kama ushuru wa vibanda hivyo.                               


  Hata hivyo alisema wamefanya jitihada mbali mbali za kuhakikisha mgogoro huo unamalizika ikiwemo kufanya vikao bila kufikia muafaka.                           


 Mgaya aliongeza kusema tangu wameanza kukaa vikao vya kutafutia ufumbuzi changa moto hiyo ya vibanda 331  ni mwaka na siku mbili umemalizika bila kupata utatuzi wake kuhusu vibanda hivyo vilivyojengwa kwa fedha zao Wafanyabiashara hao.  


 Ilidaiwa kuwa vibanda 331 vilijengwa na Wafanyabiashara hao na ndiyo maana wameamua kwenda kupiga hodi ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Mh.Serukamba na kwenda kumpigia magoti kwa sababu Viongozi wa Wilaya wameshindwa kuwasaidia,Alisema Mgaya.      

                         Suala la vibanda 331 umekuwa mwiba mchongoma unao wanyima usingizi Wafanyabiashara soko kuu Mafinga baada ya kuwekeza mitaji yao halafu kienyeji tu inatokea wanatakiwa kubomoa kwa gharama zao bila kujali mfumo wa utawala bora.                        

Wafanyabiashara hao walidai msukosuko wanaopitia wa kutishiwa kubomolewa vibanda walivyo vijenga kwa fedha zao unatishia mstakabari wa mitaji yao na kulenga kuwarudisha nyuma kiuchumi kwa kuacha kufanyabiashara na kuendelea kufikiri jinsi ya kujinasua na jinamizi hilo la kubomolewa vibanda.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS