Header Ads Widget

WENYE ULEMAVU WAPATA MAFUNZO YA USALAMA WA KAZI

Na Mwandishi wetu, Lindi

Baadhi ya watu wenye Ulemavu kutoka katika Halmashauri tatu za Mkoa wa Lindi  wamepatiwa mafunzo ya siku moja ya usalama mahali pakazi  yaliyotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahalipakazi ( Osha) Kanda ya Kusini.


Mafunzo hayo yameshirikisha walemavu kutoka Wilaya za Lindi Mjini,Kilwa na Mtama yamefanyika  katika ukumbi wa Chuo kikuu Huria uliopo Manispaa ya Lindi.

 Mhandisi Uswege Fastone   Meneja wa Osha Kanda ya Kusini  amesema wanaishukuru serikali ya Mama Samia kwakuwawezesha  pesa kwaajili ya kutoa mafunzo ya usalama Mahali pakazi na wao kuwakumbuka watu wenye mahitaji malumu kuwapatia elimu hiyo.


"Kundi la watu wenye ulemavu ni kundi lililosahaulika hawapati hizi fursa zakupata elimu kama hii ya Usalama Mahali pakazi

Tunaishukuru serikali kwa kutupatia pesa za kutuwezesha kuja kufanya mafunzo.


Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwafundisha kuhusu usalama mahali pakazi pia tutawapima afya kwa washiriki waliopo hapana vikundi vilivyopo vitapata usajiri bure,Watu wenye mahitaji maalumu ni makundi aliyosahaulika kwa muda mrefu  kwamfano wenye ulemavu hawana elimu ya usalama mahali pakazi  tumewakusanya ili wapate elimu ya usalama kwao wenyewe  pia kwa jamii inayowazunguka   ndugu zao  na familia zao. 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamewashukuru Osha kwakuwapatia mafunzo pia wamesema itawasaidia kutambua usalama wao wakati wa ufanyaji wa kazi zao.


Zuhura Meza amesema  mafunzo ni mazuri pia   yatawasaidia kujua afya zao na  kuchukuwa tahadhari wakati wakifanya kazi zao na kujua kama kazi wanazozifanya ni sala.


"Tunaishukuru serikali kwa kutukumbuka sisi watu wa kusini kwa upande wangu na kwa niaba ya walemavu wenzangu natoa shukrani kwa serikali ya Mama Samia na kwa watu wa Osha  "amesema Hamadi Shaibu  mshiriki wa mafunzo .


Mafunzo hayo yalifunguliwa na  Katibu Tawala kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi Herieti Kalua  abaye alikiri mafunzo hayo kama watayazingatia yataenda kuwasaisia .


"Niwashukuru sana Osha kwa haya mafunzo waliyo yatoa, Niwashauri vijana kujiunga katika makundi ili serikali iweze kuwasaidia kwa ukaribu.


Wenzetu Viziwi wanachangamoto ya mawasiliano  niwashauri Serikali iongeze walimu  wa Lugha ya Alama  ili waweze kuwasaidia wenzetu wenye changamoto hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS