Header Ads Widget

SERIKALI YABORESHA HUDUMA ZA TIBA KWA WENYE URAIBU DAWA ZA KULEVYA

 


Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima app Dodoma

SERIKALI imeendelea kuboresha  huduma za tiba kwa watu wenye uraibu wa dawa za kulevya katika kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo kwa kutoa tiba kwenye vitengo vya afya ya akili vyilivyopo katika hospitali za Wilaya, Mikoa na rufaa nchini. 


Akiongea na waandishi wa habari Leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya mwaka 2023,Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama amesema kwa kipindi cha mwaka 2023 jumla ya waraibu 903,062,wanaume wakiwa 470,324 na wanawake 432,738 walipatiwa huduma ya tiba ya uraibu wa dawa za Kulevya. 


Aidha amesema dawa hizo ni kama vile bangi, Mirungi, Heroine, cocaine na vilevi aina ya pombe na sigira katika vitengo hivyo.


Amesema baadhi ya watu wenye uraibu walibainika kutumia dawa za hospitali zenye asili ya Kulevya kama vile valiam, Pethidine, na Tramadol, Hali iliyosababishwa na kukosekana na kupanda kwa bei ya dawa za Kulevya mitaani. 


" Matumi ya dawa za Kulevya ya mekuwa ni moja ya tishio la afya ya jamii duniani ambapo upinguzaji wa madhara yanayosababishwa na matumizi ya dawa za Kulevya moja ya mkakati muhimu katika lupambana na tatizo la dawa za Kulevya nchini, " Amesema Mhagama

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini(DECA) Aretas Lyimo amesema kuwa katika kuhakikisha matumizi na biashara ya dawa za kulevya zinazuiliwa nchini serikali imenunua bodi itakayokuwa inakagua. 

Amesema Boti hiyo itakuwa inafanya kazi usiku na mchana katika Ku hakikisha dawa za kulevya haziingia ndani ya nchi yetu kupitia mandari. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI