Header Ads Widget

AKAUNTI CHAMA CHA WALIMU BANKI NMB YAFUNGWA

 

NA ATUKIO DAIMA App, DODOMA

AKAUNTI ya Chama Cha Walimu nchini (CWT) iliyopo Benki ya NMB imefungwa imefahamika.


Taarifa za kufungwa kwa akaunti hiyo zimetolewa na Rais wa CWT, Leah Ulaya jijini Dodoma jana Oktoba 13, 2023 ambapo alisema alipofika Makao makuu ya chama hicho Mtaa wa Jamhuri Dodoma alikuta wateja wa chama hicho wakiwa wamekwama kupata fedha zao  kwa madai kuwa akaunti ya chama hicho imefungwa na benki ya NMB.


Amesema; awali akaunti hiyo ilikuwa Benki ya MCB kabla ya kuhamishiwa NMB baada ya kutokea matatizo kama hayo ya kufungiwa akaunti yao bila taarifa zozote za msingi.


“Tulihamisha akaunti hiyo baada ya kukumbana na matatizo kama hayo kwa kigezo cha barua kutoka kwa mmoja wa waliowahi kuwa viongozi wa chama chetu aliyeondoshwa na kamati Kuu ya CWT na sasa amefungua kesi mahakamani akipinga kuondoshwa kwake.”amesema Leah


Leah alisisitiza kuwa Halmashauri Kuu ya CWT iliyokaa mwishoni mwa mwezi uliopita ilibariki kwa kauli moja kuhamisha akaunti ya MCB kwenda Benki ya NMB. 


Msemaji wa benki ya NMB, Vincent Mnyanyika  alipotafutwa kuthibitisha habari hizi simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa.


Kutokana na kadhia hiyo, aliyodai inakwamisha Chama cha Walimu, Reah amemuomba Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati suala hilo ili chama hicho kisiwe mateka kwa wanaotaka kukihujumu.


“Tunaomba viongozi wetu wakuu Rais na Waziri Mkuu ambaye kitaluma ni mwalimu kuingilia kati ili chama chetu kiwe na amani na utulivu kwani mahasimu wetu ambao waliondolewa kwa mujibu wa sheria wamesuka mbinu chafu ili kukwamisha utendaji wa CWT”amesema Leah.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS