Header Ads Widget

WADAU WA USHOROBA MTWARA WAOMBA KUHARAKISHWA UJENZI WA RELI

Na Mwandishi wetu, Mtwara

Wadau wa kamati ndogo ya watalaam  ya ushoroba wa maendeleo ya mtwara ambao wameshauri serikali kuunganisha miundombinu ya usafirishaji  na mingine kama vile barabara,  madaraja badari,viwanja vya ndege na reli sambamba na mawasiliano ya simu.


Akifungua mkutano  huo Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, kwa Niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Devotha Gabriel amesema kuwa Serikali iko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara yanakuwa rafiki na yanayovutia ili uwekezaji utakaofanyika kuwa wenye matokeo chanya kwa wawekezaji.

amesema kuwa sambambaa na kushiriki katika uwekezaji katika ushoroba wa Mtwara hususan uwekezaji katika reli ya Mtwara hadi Mbamba bay na matawi ya Liganga na Mchuchuma.


‘‘Tunatambua umuhimu wa ushirikiano baina ya Serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo, na jamii nzima katika kufanikisha malengo yetu. Hivyo basi, napenda kuwahimiza nyote mshiriki kikamilifu katika majadiliano ya leo kwa kuleta mawazo na mapendekezo yenu yenye tija’’

‘‘Napenda kutoa pongezi kwa TPA kwa kazi wanaoifanya katika bandari ya Mtwara ambapo nimefahamishwa kuwa, usafirishaji wa Korosho kupitia bandari hii umeongezeka mara dufu na kuifanya bandari hiyo kupitisha zaidi ya asilimia 90 ya korosho yote inayosafirishwa kwenda nje ya nchi ambapo pamoja na shehena nyingine, hatua hiyo imeifanya bandari ya Mtwara kuweza kuhudumia shehena zaidi ya Milioni moja na laki sita kwa mwaka 2022/23’’


Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA ambaye amemwakilisha  Mkurugenzi Mkuu wa Bandari  Mhandisi Juma Kijavala amesema kuwa ili kwenda na kasi ya uwekezaji mkoani mtwara bandari imejipanga na imeongeza mitambo na vifaa vya kushusha na kupakia mizigo.

“Kwa sasa bandari imefanya maboresho makubwa kwakuleta mitambo mikubwa yenye uwezo wa kuhudumia tani 163 lakini pia tunazo mashine za kushusha na kupakia mizigo pia tunazo tags mbili ambazo zinafanyakazi ya kutoa meli na kuingiza ambapo hapa tunajadili kabla msimu haujaanza  tuangalie changamoto tuzitatueje katika msimu msimu ujao tunahitaji ufanisi uongozeke katika bandari yetu” amesema Kijavala

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS