Header Ads Widget

WADAU WAFUNGUKA MAZITO KUHUSU TIGO PESA KIBUBU

 

Wateja wa Tigo Waipongeza Tigo Pesa Kibubu, Bidhaa mpya kutoka Tigo ya Kuweka Akiba kupitia simu za mkononiNa Mwandishi wetuWateja wa Tigo Pesa nchini wameisifia bidhaa mpya ya kidigitali ya kutoa huduma za kifedha kutoka Tigo Tanzania maarufu kama Tigo Pesa Kibubu, wakisema kwamba hii ni bidhaa ya kimapinguzi ambayo itabadilisha namna wanavyofahamu na kushughulikia akiba zao.   Wakiongea katika nyakati tofauti katika vyombo vya habari wakizungumzia bidhaa iliyozinduliwa hivi karibuni na kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Bank of Afrika (BOA), wateja hao wamekubali kwamba Tigo Pesa Kibubu ni huduma itakayo leta mabadiliko katika namna ambavyo watakavyokuwa wanaweka akiba zao siku zijazo.  Tigo Pesa Kibubu kwa mujibu wa kampuni ya Tigo, ni mfumo wa kidigitali wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambao unawawezesha wateja kuweka akiba na kujipatia riba kupitia simu zao za mkononi.  Vile vile, huduma hii inawawezesha wateja wa Tigo Pesa kuweka akiba ya kiwango fulani cha fedha za kielektroniki (e-money) na kujipatia kulingana na kiwango cha fedha kilichohifadhiwa.  Bwana Arbogasti Mayoo mwenye umri wa miaka 32, muuza mitumba katika soko la Kariakoo jijini Dar es salaam, wakati akitoa maoni kuhusu Tigo Pesa Kibubu alisema"  "Huduma ya Tigo Pesa Kibubu ni neema mpya imenifikia kwa sababu hapo kabla nilikuwa ninaficha nyumbani fedha kutoka kwenye biashara yangu. Nilikuwa nafikiri kwamba hazitoshi kuziweka benki, lakini baada ya kuja kwa huduma ya Tigo Pesa Kibubu, nimeamua sasa kuhamisha fedha zangu kutoka nyumbani kwenda katika mfumo mpya wa kuweka akiba ambayo ninaamini ni salama; na vile vile nitajipatia riba katika akiba hiyo.  Sita hifadhi tena nyumbani fedha ambazo ninahitaji kuziweka kama akiba". Mfanya biashara mwingine anayefanya biashara za kutembeza, bwana Morris Simanyara 28, ambaye anauza mapegi ya kusafiria katika eneo la machinga complex jijini Dar es salaam, alikuwa na haya ya kusema kuhusu Tigo Pesa Kibubu.  "Hapo awali, nilikuwa nahifadhi fedha zangu zote za biashara na za matumizi katika waleti yangu ya kawaida lakini nimehamishia kwenye Tigo Kibubu kwa sababu nina njia rahisi zaidi ya kiweka akiba yangu"  Aliongeza bwana Samanyara:  "Unafahamu kuwa waleti ya kawaida ni rahisi sana kupotea au kuibiwa, jambo linalomaanisha kwamba fedha wakati wote haziko salama lakini sasa kwa sababu ninaweka akiba yangu kwenye Tigo Pesa Kibubu, sina wasiwasi wa kupotea kwa fedha kwa namna yoyote, Tigo Pesa Kibubu inanihakikishia riba kutokana na kuendelea kudunduliza akiba yangu. Kutoka Mwaloni, moja kati ya masoko maarufu ya samaki Afrika Mashariki jijini Mwanza, Kanda ya Ziwa, tunakutana na mteja mwingine wa Tigo Pesa Kibubu akisema kwamba itabadilisha namna ambavyo yeye na wafanya biashara wenzake wa samaki walivyokuwa wanaweka akiba zao za fedha za biashara.  "Tuna kikundi kidogo ambacho kina jumuisha wefanya biashara wenzangu na hapo awali tulikuwa tunatoa mchango wa kikundi kila wiki na kumkabidhi mmoja wetu ili awe msimamizi wa hizo fedha.  Hata hivyo tumekuwa na changamoto kwenye mapato na vile vile mashaka kuhusu usalama wa fedha.  Kwa kuzinduliwa kwa huduma ya Tigo Pesa Kibubu, sasa tumeamua  kuanza kutumia mfumo huu mpya kwa sababu ni bora, salama na hauna usumbufu katika kuweka akiba na vile vile tutaweza kujipatia riba kupitia kwenye akiba zetu" alisema.  Bi Anitha Kimaro, mfanyabiashara chipukizi ameanzisha duka mjini Moshi amekuwa na maoni karibu sawa na wenzake kuhusu Tigo Pesa Kibubu.  Akibainisha kwamba hapo awali hata hakuwahi kufikiria ni njia ipi ya kuweka akiba atakayo tumia kwa sababu anaona kipato chake ni kidogo sana, Kimaro amesema Tigo Pesa Kibubu imeweza kumpatia njia nzuri ya kuweka akiba kwa sababu haiba ukomo wa kiasi gani cha fedha mteja anapaswa kuwa nacho kabla ya kuanza kuweka akiba.  "Tigo Pesa Kibubu inafaa sana katika biashara yangu hii ndogo; Tayari nimeshaanza kuitumia na ninaamini kwa kupitia huduma hii biashara yangu itakuwa yenye mpangilio zaidi". alisema bi Kimaro.  Kwa mujibu wa Angela Pesha, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Tigo Pesa Kibubu inamuwezesha mteja kuweka akiba kuanzia kiasi kidogo kama TZS 1 na kujipatia riba, ikimaanisha kwamba Wateja wa Tigo Pesa wanaweza kutumia huduma hii.  "Huduma ya Tigo Pesa Kibubu ni bidhaa ya kuweka akiba ambayo inaunganisha waleti kuu ya Tigo Pesa kwenda kwenye waleti ya Tigo Pesa Kibubu kwa madhumuni ya kuweka akiba." Alisema Pesha, akiongeza kwamba bidhaa hii imeandaliwa kuleta utaratibu mpya wa kuweka akiba katika uchumi wa Tanzania. Pesha anabainisha kwamba kwa kuwapatia wateja wa Tigo Pesa njia rahisi na bora ya kuweka akiba , Tigo Pesa Kibubu itawapatiia kiwango bora cha maisha yenye mpangilio, kuwafikia wateja ambao wako nje ya mfumo rasmi ya kibenki, hivyo kuhamasisha ujumuishwaji wa kifedha nchini.  Akibainisha kwamba utumiaji wa Tigo Pesa Kibubu miongoni mwa wateja umekuwa na mwitikio mzuri, Pesha amesema kwamba huduma hii tangu ianze kufanya kazi tarehe 2 Septemba 2021 imepokea zaidi ya TZS Bilioni 2 kama akiba kutoka kwa zaidi ya wateja 64,000 mafanikio makubwa ambayo yanaweza kuelezwa na umaarufu wake wa haraka.   Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Jumla ya Akiba za Ndani (Gross Domestic Savings) (% ya GDP) onchini Tanzania ilikuwa 34.08 asilimia katika mwaka 2020. Wakati huo huo Mfumo wa Taifa wa Ujumuishaji wa Kifedha Tanzania (-NFIF-2020) imebainisha kwambaTanzania imekuwa na maendeleo makubwa katika kuongeza fursa za watu kuweza kutumia huduma za kifedha, kwa kuongezeka kwa huduma rasmi za kifedha kufikia asilimia 65 mwaka 2017 kulinganisha na asilimia 57.7 katika mwaka 2013.

Post a Comment

1 CommentsMAGAZETIBBC NEWS