Header Ads Widget

TCRA YATAJA SABABU YA TATIZO LA INTERNET KUKOSEKANA NCHINI

 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imesema Kuna tatizo la Mfumo wa Mawasiliano ya Intaneti kwenye Mkongo wa Baharin

Kama umekosa huduma ya intaneti kwa saa kadhaa leo, tambua shida sio kifaa unachotumia bali ni tatizo la kiufundi lililotokea kwenye miundombinu ya intaneti iliyopitishwa baharini.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Jabir Bakari amelithibitisha hilo alipotafutwa na Mwananchi Digital leo Jumapili Mei 12, 2024.

"Kunaonekana kuna tatizo la kiufundi kidogo linalohusiana na 'marine cables' kwa hiyo tunajaribu kupata maelezo zaidi," amesema Dk Bakari.

Dk Bakari amesema kwa sasa wanaangalia namna ya kupata taarifa zaidi ili kujua ilipo changamoto ili kuchukua hatua.

Tatizo la mtandao wa intaneti limeanza tangu saa 4 asubuhi na hadi habari hii inapoandikwa saa 7.10 mchana huduma hiyo haijarejea.:chanzo JF


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI