Shekhe Hassan Iddi Kiburwa Shekhe wa mkoa Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
SHEKHE wa mkoa Kigoma Hassan Iddi Kiburwa amesema kuwa suala la ushoga na ulawiti ni janga kwa jamii ya watanzania hivyo amewataka watanzania kuungana kulipiga vita jambo hilo kwa nguvu.
Shekhe Kiburwa alisema hayo katika sala ya Eid El Fitr iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ujiji manispaa ya Kigoma Ujiji iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam na kusema kuwa waumini wa dinj zote wanapaswa kulipinga hilo kwa kufuata misingi ya dini zao na mila na desturi za nchi.
Alisema kuwa wazazi wanapaswa kufanya juhudi kubwa kuwalinda watoto wao kwani vitendo hivyo vimevuka mipaka na kwenda kwenye maeneo ambayo si rahisi kuamini ikiwemo mashuleni na kwenye taasisi za dini.
Katika ibada hiyo ya salama ya Eid Shekhe huyo wa mkoa Kigoma ameomba watanzania kudumisha umoja,amani na mshikamano huku akiongoza waumini kumuombea dua ya afya njema Raisi Samia Suluhu Hassa na wasaidizi wake wote ndani ya serikali ya awamu ya sita.
Akizungumza katika sala hiyo ya Eid El Fitr Mkuu wa wilaya Kigoma,Salum Kali alisema kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani waumini wa dini ya kiislam walikuwa wakifanya matendo mema hivyo kumalizika kwa mfungo huo isiwe sababu ya kurudia matendo hayo na badala yake iwe kama darasa ambalo limewafundisha ucha mungu na kufanya matendo mema.
Awali kiongozi wa taasisi ya ISUWAT, Dabas Khalfan Kiumbe aliwahimiza waislam kuishi kwa umoja na kupendana na kushirikiana katika kufanya mambo mbalimbali kama ambavyo sala hiyo ya Eid imesaliwa na viongozi wa dini ya kiislam kutoka madhehebu mbalimbali.
Mwisho.
0 Comments