Header Ads Widget

NAMNA LIGI YA ULAYA ILIVYOSISIMUA NA MAGOLI LIKUKI

 

Manchester City na Real Madrid zilifunga mabao sita katika mchezo wa kusisimua na kuhitimisha robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mkondo wa kwanza kwa sare ya 3-3 katika uwanja wa Bernabeu.

Kikosi cha Pep Guardiola kiliongoza katika dakika ya pili wakati Bernardo Silva alipopiga mkwaju wa wa adhabu ndogo kutoka umbali wa yadi 25 lililompita mlinda lango Andriy Lunin.

Mshambulizi mawili ambayo hayakuzaa matunda yaliwafanya mabingwa mara 14 wa ligi ya mabingwa Ulaya Real Madrid kuutawala mchezo. Mkwaju wa mbali wa kwanza wa Eduardo Camavinga ulimgonga Ruben Dias na kutinga. komiani katika kona ya mbali ya goli la Stefan Ortega, kabla ya Rodrygo kuichsmbua ngome ya walinzi wa City na kutikisa nyavu kupitia kisigino cha Manuel Akanji.

City walikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira ugenini katika dimba la Bernabeu lakini walishindwa kuingia katika eneo la hatari la wapinzani - hadi Phil Foden alipoachia mkwaju mkali na kuiandikia City goli la kusawazisha.

Kiungo huyo wa kati raia wa England alikuwa pembeni mwa uwanja lakini alipata nafasi nje ya eneo la hatari na kugeuka na kuwa moto katika kona ya juu na hivyo kuirejesha City mchezoni

Muda mfupi baadaye beki wa kushoto Josko Gvardiol aliachia shuti kali la mguu wa kulia na kufunga bao lake la kwanza tangu alipojiunga na City kutoka RB Leipzig msimu katikati mwa mwaka jana.

Hata hivyo, Madrid ilisawazisha kwa mkwaju mkali wa guu la kulia kutoka kwa Federico Valverde.

Kane amefunga mabao mengi kwenye Premier League dhidi ya Arsenal (14) kuliko mtu mwingine yeyote


Katika mechi nyingine Muingereza Harry Kane alirejea kaskazini mwa London akiwa na goli wakati matumaini ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa Ulaya yakiachwa mashskani baada ya kutoka sare ya 2-2 na Bayern Munich katika mechi ya robo fainali ya kwanza katika uwanja wa Emirates.

Kane, ambaye ni mfungaji bora wa mabao wa Tottenham, alipata mapokezi ya hasira kutoka kwa mashabiki wa Arsenal, ambao walishuhudia Gunners wakianza vizuri wakati Bukayo Saka alipowatanguliza baada ya dakika 12 tu za mchezo

Bayern walijizatiti na kuijiepusha na mbaya kimchezo inayowakabili katika ligi ya nyumbani kwao Bundesliga na kuugeuza mchezo huo kabla ya mapumziko wakati mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry aliposawazisha dakika sita baadaye.

Leandro Trossard amefunga mabao mawili katika mechi zake mbili zilizopita akiichezea Arsenal


Wasaa wa Kane ulifika wakati William Saliba alipomwangusha Leroy Sane wakati wakikimbizana baada ya dakika 32za mchezo. Nahodha huyo wa England alisonga mbele kwa mkwaju wa penalti na kuwanyamazisha mashabiki waliokuwa wakimzomea kwa bao lake la 15 katika mechi 20 dhidi ya Arsenal.

Kikosi cha Mikel Arteta hakikuwa katika ubora wake wa kawaida, lakini mchezaji aliyetokea benchinla wachezaji wa akiba, Leandro Trossard alinufaika na kazi bora ya Gabriel Jesus na akasawazisha

Arsenal walihisi kuwa walistahili kupata penalti katika sekunde za mwishoni mwa mchezo, lakini mwamuzi aliamuru mchezo uendelee wakati Saka alipogaagaa chini wakati alipokabiliana mlinda lango wa Beyern, Manuel Neuer.

The Gunners walikuwa na bahati pia ya kutopigiwa penalti mapema katika kipindi hicho, wakati Gabriel alipochukua mpira kwa mikono baada ya mwamuzi kuashiria kupigwa kwa goli kiki.

Wachezaji kadhaa wa Bayern walilalamika wakati huo lakini mwamuzi alisimamia uamuzi wake.Mechi za mkondo wa pili baina ya timu zilizocheza jana Jumanne zitapigwa juma lijalo Jumatano, Aprili 17.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI