Na Fredrick Siwale - Matukio Daima APP - Mufindi.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imelitaifisha gari lenye namba za usajili T.803 CVW Landcuiser VXR , V8 inayomilikiwa na Said Hassan mkazi wa Tabata Dar es salaam, kwa kosa la kusafirisha Wahamiaji haramu raia wa kutoka Nchini Ethiopia.
Hayo yamesemwa nje ya ukumbi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi katika Halmashauri ya Mji Mafinga na Mwendesha Mashtaka mkuu wa mkoa wa Iringa (NPS)
Akizungumza na Vyombo vya habari. Bw.Namkambe alisema uamuzi huo umetolewa April 12 ,2024 na Mahakama ya Wilaya ya Mufindi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Mh.Benedick Nkomola .
Mwendesha Mashtaka mkuu mkoa wa Iringa Bw.Namkambe alisema kesi hiyo namba 9406/2024 ilifikishwa Mahakamani kwa mara ya pili tangu Washitakiwa hao wakamatwe April 06 /2024 eneo la msitu wa Luganga kata ya Ifwagi Wilaya ya Mufindi wakiwa wametelekezwa katika Shamba la mahindi .
Washitakiwa hao awali walishitukiwa na Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani Kituo cha Mafinga Wilaya ya Mufindi Sajenti Beruto akiwa katika kutekeleza majukumu yake ya kazi alipobaini dereva wa gari Landcuiser VXR - V8 likiwa limebandikwa namba za Serikali zilizo kuwa zinasomeka STL 3999 likiendeshwa mwendo kasi na hatarishi huku likiyapita magari mengine bila tahadhari na kulisimamisha .
Baada ya kusimama inadaiwa dereva wa gari hilo alianza kuomba msaada ili aruhusiwe kuendelea na safari, na kuongeza kuwa umakini wa Askari huyo aliendelea kulichunguza gari na kubaini kuwa lilikuwa limebeba Watu waliodhaniwa kuwa ni Wahamiaji haramu .
Ilidaiwa dereva wa gari hilo ambaye hajafahamika aliamua kuliondoa kwa kasi na kufika eneo la Majinja alikata kushoto nje ya barabara kuu ya Mafinga Njombe.
Sajenti Beruto inadaiwa alijuliwajulisha Askari wenzake na kuanza kulifuata gari hilo na kufanikiwa kulikuta likiwa limetelekezwa Dereva akiwa amelizima na kutokomea kusikojulikana akiondoka na funguo za gari pamoja namba za STL 3999 na kubandika namba zake halisi za T.803 CVW na kulitelekeza kwenye shamba la mahindi pamoja na Wahamiaji haramu 16.
Ilidaiwa kuwa Watuhumiwa walichukuliwa pamoja na gari kuvutwa hadi kituo cha Polisi Mafinga mjini kwa hatua zaidi za kisheria na kufikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza ambapo walisomewa shitaka lao na kila mmoja kukili kosa.
Shitaka waliloshitakiwa nalo ni kuingia Nchini bila kibali kifungu
45 ,1 ,i & ii ndogo na 2 sura ya 54 ya Uhamiaji ya mwaka 2016.
Washitakiwa walikumbushwa shitaka lao kwa mara ya pili April 12 ,2024 Washitakiwa walikili tena na Mahakama kuwatia hatiani na walipopewa nafasi ya kujitetea kila mmoja aliomba msamaha na kuomba Mahakama iwasamehe.
Baada ya kukili kosa lao Mwendesha Mashtaka mkuu mkoa wa Iringa Bw.Namkambe kupitia kifungu 45 1,i & ii ndogo 2 sura 54 ya Uhamiaji aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo la kuingia Nchini bila kibali.
Akisoma hukumu Mh.Nkomola alisema Mahakama inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila mshitakiwa ama kulipa faini ya sh.500,000 (Laki tano) kila mmoja na wakimaliza adhabu watakabidhiwa Mamlaka husika ili warudishwe Nchini kwao Ethiopia.
Baada ya hukumu hiyo kutolewa Mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Bw.Namkambe aliiomba Mahakama kuitaifa gari hiyo T.803 CVW - VXR V8 na kuikabidhi kwa Msimamizi wa mali za Serikali kwa kunukuu kifungu 351 (1) a & b ndogo muongozo sura 20 rejeo la mwaka 2022/24 .
Akihitimisha kutoa hukumu hiyo Mh.Nkomola alisema kupitia kifungu 351 (1) a&b ndogo muongozo sura 20 rejeo la 2022/2024 gari hilo lenye namba za usajili T.803 CVW Landcuiser VXR - V8 Mahakama imelitaifisha na kulikabidhi kwa Msimamizi wa mali za Serikali.
0 Comments