Header Ads Widget

MLIMA WAPOROMOKA WANAFUNZI ZAIDI YA 200 WANUSURIKA KIFP


Picha hii ya mtandaoni haina uhusiano na habari hii.

Wanafunzi 200 wa Shule ya Msingi Generation iliyopo katika Kata ya Itezi Jijini Mbeya, wamenusurika kifo baada ya mabweni waliyokuwa wanaishi kufukiwa na tope lililotokana na kuporomoka kwa Mlima Kawetele kutokana na mvua inayoendelea kunyesha.


Tope hilo limefunika pia nyumba 20 za makazi ya Wananchi na kusababisha zaidi ya Wananchi 200 kukosa makazi huku dalili zikionesha Mlima huo kuendelea kumeguka.


Tukio hilo limetokea asubuhi wakati baadhi ya Wananchi wakiwa ndani ya nyumba na wengine wakiwa Makanisani huku Wanafunzi wa Shule ya Generation wakiwa shuleni hapo ambapo waliondolewa kabla mabweni yao hayajafunikwa


Diwani wa Kata ya Itezi, Sambwee Shitambala amesema tukio hilo limesababishwa na uharibifu wa mazingira kwenye Mlima huo hasa ukataji hovyo wa miti, shughuli za kilimo na ujenzi wa makazi maeneo ya Milimani na kwamba kuna baadhi ya nyumba Wananchi hawakuokoa kitu chochote kutokana na kukimbia kujiokoa baada ya kusikia kelele za maporomoko hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameagiza Wananchi watakaokosa makazi watafutiwe maeneo salama na akaagiza masomo kusitishwa katika Shule hiyo pamoja na ya Mary's ambayo iko jirani

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI