Header Ads Widget

WANAWAKE OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA WAWAKUMBUKA WAGONJWA DODOMA

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma

OFISI ya Taifa ya Mashtaka imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya matibabu kwa wagonjwa walilazwa kwa muda mrefu kwenye hospitali ya rufaani ya mkoa wa Dodoma.


Wakili wa serikali Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Chivanenda Luwingo, akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa amesema Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 8 mwaka huu msada huo ni sehemu ya matendo ya huruma wakati huu wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Amesema kuelekea siku hiyo ya wanawake Duniani wanawake wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wameenda kuona changamoto zilizipo kwa wagonjwa na kubaini uwepo wa wagonjwa wa muda mrefu ambao gharama za matibu kwao zimekuwa kubwa.


"Leo hii tutawalipoa gharama matibabu wagonjwa hawa wa muda mrefu watano pamoja na mtoto mmoja ambaye anahitaji gharama za upasuaji na dawa kwa muda wa siku saba jumla ya gharama za matibabu yote ni 900,000"alisema

Pia, alisema pamoja kugharamia matibabu hayo pia wametoa vitu mbalimbali kwa manusura wa ukatili wa kijinsi ikiwemo watoto waliyupwa wa wazazi wao.


"Tumetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto manuscript wa ukatili ambao waliputwa na wazai wao hvyo wanahitaji vitu kama nepi, maziwa pamoja na dawa mbalimbali lakini pia tumetoa msaada wa sabuni na mafuta jumla gharama zote.inakuwa ni Sh. milioni mbili"alisema

Muuguzi Mfawidhi wa hospitali ya rufani mkoa wa Dodoma Stanley Mahundo, aliishukuru Ofisi ya Taifa ya Mashtak kwa msaada huo ambao utakwenda kusaidia wagonjwa wenye uhitaji.


"Tunaishukuru sana Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa msaada huu na tunaahidi kuwa tutahakikisha msaada huu unawafikia walengwa na nitoe wito kwa watu wengine kujitoa kusaidia wagonjwa kama hawa"alisema

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI