Na; Matukio Daima App
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo kidunia ufanyika Machi 8, kila mwaka, Mratibu wa Mtandao wa Wanawake Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (CWHRD) Hilda Stuart amesema kumekuwepo na wimbi la Wanawake wengi wenye hofu ya kujihusisha na siasa kutokana na madhira mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwakumba baadhi ya Wanawake.
Akizungumza leo Machi 6, 2024 kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake ambayo yaliandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa haki za Blbinadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na CWHRD, kupitia mjadala uliondaliwa kwa kuwakutanisha wakurugenzi zaidi 50 kutoka taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali ikiwa ni siku mbili kabla ya siku rasmi ya maadhimisho hayo, amesema kuwa wawake wamekuwa na hofu wa kuwania nafasi za kisiasa ambazo uamua hatima yao ya maendeleo.
"Kuna Haki nyingi za Wanawake bado hazijatimizwa kwa mfano utekelezwaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Nchi imeridhia bado utekelezaji wake ni wa pole pole"
Amesema jambo hilo ni kikwazo ambacho kimekuwa kikifanya ushiriki wa Wanawake kuwa chini, kikwazo kingine chaambacho amebainisha ni Wanawake kushindwa kushiriki ipasavyo kwenye siasa ni aina ya mifumo ambayo bado inaendelea kuweka mazingira magumu kwa Mwanamke.
Pia amesema kuwa kumekuwepo na mazingira ya 'unyanyasaji wa kingono' kwenye siasa ambayo ni kikwazo kwa Wanawake wengi kukosa mwitikio wa kushiriki kwenye kuingia kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi.
"Kuna unyanyasaji wa kingono, wengi wanaogopa ni kwa taarifa zilizopo. Mimi pia nimefanya kazi na Wanawake ambao ni wanasiasa nakutana nao wengi ambao wanajaribu kugombea nafasi wanakutana sana na hayo matukio ya unyanyasaji wa kingono"amesema Hilda Stuart
Ameongeza kuwa nafasi za ushiriki zinakuwepo kwa ajili yao lakini mchakato wa kufikia nafasi ndipo Wanawake wengi wamekuwa wakihofia kutokana na kukutana na madhira.
Hata hivyo amepongeza jitihada za wadau na Serikali kubaini changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye michakato ya kisiasa hususani kwenye uchaguzi "Nashukuru Bunge letu na Serikali ya Tanzania kukubali kwamba kosa la unyanyasaji wa kijinsia kipindi cha uchaguzi hama kwenye siasa limeingizwa kama kama kosa kwenye uchaguzi. Sasa hilo tunakiwa kuwaelimisha wananchi wanaotaka wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwamba kuna kitu ambacho kinatulinda kwa sasahivi"
Aidha Afisa Programu THRDC, Wakili Nuru Maro amesema THRDC imekuwa na utamaduni wa kuandaa mijadala mbalimbali kwenye siku ya Wanawake inayolenga kutambua na kukuza jitihada za utetezi wa haki za binadamu unaogusa Wanawake kwenye nyanja mbalimbali.
"Sisi kama Mtandao imekuwa ni utamaduni wetu kila mwaka kusherekea siku ya Wanawake kwa kufanya kitu ambacho ni tofauti ambacho kinaenda kuigusa jinsia ya kike" amesema Wakili Nuru Maro
Amesema kuwa kwa miaka iliyopita wamefanikiwa kukutana na makundi mbalimbali ya Wanawake ikiwemo Watetezi wa haki za binadamu wenye ulemavu pamoja na kuadhisha siku hiyo na Wanawake ambao wamedumu kwa muda mrefu katika harakati za utetezi wa haki za binadamu
Akizungumzia maadhimisho ya mwaka huu yaliyofanyikia kwenye ukumbi PSSSF Jijini Dar es salaam yenye dhima isemayo "Wekeza kwa Wanawake harakisha Maendeleo", amesema kwa mwaka huu wamekutana na wakurugenzi Wanawake Watetezi wa haki za Binadamu zaidi ya 50 huku wakiamini bila kuwekeza kwa Mwanamke inaweza kuwa kikwazo cha kufikia maendeleo endelevu.
"Wakurugenzi kupitia taasisi zao wamekuwa wakiwekeza kwenye miradi mbalimbali inayogusa masuala ya jinsia, haki za Wanawake, haki za kijamii, haki za kisiasa, haki za kiuchumi ili kumkomboa Mwanamke na kuhakikisha Dunia sehemu yenye usalama kwa watu wote"amesema Wakili Nuru Maro
Amesema kuwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa mijadala iliyogusa maeneo yafuatayo, Uwekezaji wa miradi ya Wanawake na mashirika ya Wanawake, Masuala ya tabia ya Nchi, Maendeleo ya kidigtali, haki za kiuchumi
"Kwenye mkutano huu tutatoka na maazimio ambayo wakurugenzi wataenda kuyatekeleza Mwezi mzima wakati wakisherekea siku ya Wanawake, lakini tunatambua mwaka huu katika ngazi ya umoja wa mataifa unafanyika mkutano wa Tume ya Hali ya Wanawake utakaoanza March 11, 2024 New York, nasisi tunao wawakilishi ambao katika mkutano huu tutatoka na maazimio ambayo tutatoa taarifa yetu kule inayoonesha Tanzania hali yetu ipoje"amesema Wakili Nuru Maro
0 Comments