Header Ads Widget

SIKU TISA CHADEMA MAANDAMANO AWAMU YA PILI NCHINI

Na Mwandishi wetu, Mtwara, Matukio Daimaapp. Mtwara

Chadema wajipanga siku tisa za maandamano awamu ya pili yakayofanyika kwenye makao makuu ya mikoa yote nchini kuanzia Aprili 22, 2024.


Maandamano hayo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe baada ya kumaliza maandamano makubwa yaliyofanyika kwenye majiji ya Dar es salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza.

Amesema kuwa wanaingia katika awamu ya pili na kuita kuwa ni wiki ya maandamano nchini ambapo yatafanyika katika makao makuu ya mikoa yote nchini baada ya kusitisha ili kupisha mfungo wa kwaresima pamoja na mwezi mtukufu wa ramadhani.


Mbowe amesema kuwa wanafanya maandamano hayo kwakuwa hawaridhishwi na mwenendo mzima wa serikali ya CCM   hivyo kuja na azimio la Mtwara  baada ya vikao vya kamati vilivyokaa kwa siku nne mfululizo kujadili mustakabali wa nchi yetu.

 “Chadema imejiridhisha kuwa chama cha Mapinduzi (CCM) haina mbinu, utashi wala dhamira ya kupunguza gharama za maisha  ndio maana sisi wenye uwezo wa kufikiri na kubuni tumetoa mapendekezo yetu ili yafanyiwe kazi na kusaidia kupunguza ukali wa maisha kwa watanzania”


“Hata hivyo umechoka kuvumilia dharau na ukaidi wa CCM  katika kukataa madai ya haki ya kupata katiba mpya mfumo mpya wa kidemokrasia wa uchaguzi utakaoboresha mfumo wa kiuchumi utakaoleta nafuu ya maisha kwa watanzania”

Katika hatua nyingine amesema kuwa hakuna watu wanaoathirika kwenye hoja ya afya kama wanawake na hawa ndio wanaotunza watoto sisi kama chama tutatoa tamko siku ya wanawake duniani ambapo tutatoa tamko rasmi kwa sasa tunaikata serikali iwasikilize watoa huduma itambue kuwa kuwatunishia misuri kunaua watanzania wasio na hatua katika utaratibu wa dharura na haraka wasilazimishe watu watoe huduma kwa gharama hizo.


"Msiwalazimishe waotoa huduma watoe huduma ambazo sio bora inayolingana na pesa waliyotoa watoe huduma bora ambayo itawasaidia watanzania

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI