Header Ads Widget

MADIWANI NANYAMBA WAJIFUNZA BAGAMOYO UKUSANYAJI WA MAPATO

Na Mwandishi wetu Matukio Daimaapp, Bagamoyo

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mji Nanyamba wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ili kujifunza ukusanyaji wa mapato na namna bora ya kutelekeza miradi ya maendeleo. 


Akizungumza mara baada ya kuwasili Wilayani humo Mkurugenzi wa Mji Nanyamba Thomas Mwailafu amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kujifunza ili kuona nini kinachofanyika katika Halmashauri zingine.


Amesema kuwa ziara hiyo wanaangalia mapato wanatumia mbinu gani kuyakusanya na utelekezaji wa miradi inaweza kutekelezwaje ili kuwapa nafasi madiwani wakati wa kufanya maamuzi.

"Hii ni ziara ya kujifunza ambapo tunaamini kuwa tukiotoka hapa tunaenda kusimamia vizuri mikataba ya mawakala  na kubuni ubunifu wenye tija kwa halmashauir yetu lakini pia tumejifunza mambo mengi tumeona namna wanavyokusanya mapato kwakutumia zabuni tofauti na sisi hii kwetu ni fursa”


"Huku tumeona fursa ambazo tunaweza kuzibadilisha na kuwa fursa ikiwemo madini ya mchanga ukusanyaji wa mapato kwa kutumia zabuni ambapo tukiongezea na fursa ya kilimo na maghala tutakuwa tumepiga hatua na kuongeza mapato”


“Baada ya mafunzo haya tunaenda kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha vilivyopo ili tutoke kwenye mapato ya ndani shilingi bilioni 2 ili twende kwenye mapato ya shilingi bilioni 3-4 ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii uwe mzuri hasa kwenye kilimo, afya na elimu” amesema Mwailafu  

Kwa upande wake Mkurugenzi Bagamoyo Shauri Selenda amesema kuwa ugeni huo ni wakubadilishana uzoefu ili kuboresha makusanyo na utelekezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


“Tumepokea ugeni ambao wamekuja kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo ambapo  tumeongeza kutoka 2019 ambapo tulikuwa tunakusanya shilingi Bilioni 3 hadi bilioni 6 kwa sasa yaani ongezeko la asilimia 100 ambapo kila mwaka tunaongeza shilingi bilioni1”


Nae Fatuma Jaluo Diwani Vitimalum Taarafa ya Kitaya Mji Nanyamba amesema kuwa wamefika kujifunza ili kuboresha mapato.


“Unajua ujio wetu tumejifunza na tumeejifunza mengi na tukienda kutelelekeza itatupa nafasi ya kufanya vizuir zaidi mfano madini ya mchnag sisi tuliokuwa tunaona kawaida kumbe ni bishara kutembea kutasaidia kuboresha halomahashauri yetu” amesema Jaluo

Hadija Livanga Diwani Viti maalum Halmashauri ya Mji Nanyamba amesema kuwa ukusanyaji wa mapato umekuwa mdogo lakini kupitia mafunzo haya tunaenda kuboresha zaidi.


“Umeona namna walivyokusanya mapato ambapo wanamtumia mzabuni sisi hatukuwa tunafanya hivyo tulikuwa tunawatumia watendaji wa mitaa na vijiji  lakini tukipata mzabuni tutafanikiwa zaidi”


Nae Sophia Champunga diwani wa vitimaalum amesema kuwa tutaboresha makusanyo na tutaongeza fursa zaidi za kimaendeleo katika mji wetu.


“Tukitumia mzabuni tutakuwa nae siku zote hadi mwisho wa wiki yaani hawata poteza siku hii itatunyanyua zaidi kimapato na itaboresha mapato  ndio maana tumejifunza na tunarejea kufanya vizuri zaidi kwenye kuongeza mapato”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI